tag:blogger.com,1999:blog-5534204562849596072.post1318109934497419819..comments2013-03-01T17:32:00.279+00:00Comments on Uk & Tanzania News, Photos and Comedy: Ally Muhdinhttp://www.blogger.com/profile/02763878463249203643noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-5534204562849596072.post-66627013354295416822010-05-03T15:51:51.709+01:002010-05-03T15:51:51.709+01:00Si viongozi wengi wanaosisitiza wananchi wapendane...Si viongozi wengi wanaosisitiza wananchi wapendane; iwe Bongo, iwe kimataifa. Tamko la namna hii litakuwa limetoka mdomoni mwa mwanamke. Baadhi ya wanawake madarakani huwa na kile wataalamu waitacho “inter personal skills” ambazo husaidia kuongoza kwa kuzingatia mawasiliano ya karibu zaidi na waongozwaji.<br />Chunguza. <br />Kati ya matatizo ambayo yamechangia wananchi kutoamini taasisi mbalimbali za kiserikali (ukiwemo ubalozi London) miaka iliyopita ni kuwa na viongozi wahuni, wasioaminika au bla bla, maneno matupu. <br />Katika muda mfupi Mama Maajar kajitahidi, kujaribu kuondoa usongo huu. Kati ya aliyofanya ni mathalan, kukutana na wananchi mara moja kwa mwezi, kusukuma vyama mbalimbali ikiwepo TAWA na mikutano miwili ya Diaspora London. Si ajabu alipigiwa makofi juzi. Na si ajabu wanawake wengi wakamwona kama mtu wa mfano (role model). Ila ile sherehe ilikuwa na tatizo la kukosa “ratiba” maalum. Hotuba nyingi, muziki kukatishwa katishwa, bendi kunyamazishwa na kutopiga zaidi miziki ya kwetu ya Kiswahili, nk.<br /> Hili ni tatizo kubwa sana kwetu Watanzania. Kujifanyia mambo kiholela. Tutegemee siku zijazo udhaifu huo utarekebishwa maana Balozi keshapanda mbegu.Kitotohttp://www.kitoto.wordpress.comnoreply@blogger.com