BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday 30 May 2010

Lovely Gamble yazinduliwa Rasmi nchini Uingereza

Kikundi cha kutengeneza Tamthilia Urbun Purse wamezindua rasmi tamthilia ya "Lovely Gamble" katika mji wa Reading, nchini Uingereza.

Tamthilia hiyo inayohusu Mapenzi, Muziki, Usaliti na Uongo imetungwa na Frank Eyembe pamoja na Alan Kalinga.

Mhariri wa tamthilia ya "Lovely Gamble" Baraka Baraka amesema wamejaribu kutengeneza tamthilia hiyo katika kiwango cha kimataifa ili kuweza kulingana na tamthilia nyingine zinazoonyeshwa duniani.

Mtunzi wa tamthilia hiyo Frank Eyembe amesema jina la tamthilia limejieleza kwani kila kitu kinachohusiana ya tamthilia wamecheza pata potea kwani hawakujua jinsi gani wataweza kufikia hapo walipofikia.

Matukio na mambo yaliyofanyika katika tamthilia hiyo hayajalingana na tamthilia nyingine.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa tamthilia hiyo Mwenyekiti wa TA John Lusingu amesema amefurahishwa na kitendo cha Watanzania kujitokeza na kuonyesha kuwa na uwezo wa kufikia mbali katika utengenezaji Tamthilia.

Akiongea kwa niamba ya Balozi Maajar, mgeni rasmi Amos Msanjila alitoa shukrani kwa waandaaji na watayarishaji wa tamthilia hiyo kwa kukumbuka kama kuna ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kuweza kushikiana nao katika hafla mbalimbali.

Bw. Msanjila alifurahishwa sana na kazi waliyoifanya Watanzania walio nje ya nchi kwa kuweza kujitafutia ajira na kuitangaza nchi yao katika masuala ya tamthilia.

"Jamani tupende vyetu" miaka ya 90 hatukuwa na uwezo kama tuliofikia hivi sasa. Alisema Msanjila.

Amewashauri Watanzania wasiogope Uthubutu, wakubali kurekebishwa na tupeane moyo.

Akifunga hafla ya tamthilia hiyo, Bw. Eyembe alitoa shukrani za dhati kwa Watanzania wote waliojitokeza na kutoa michango katika kufanikisha kuitangaza tamthilia hiyo.

Pesa zitakazopatikana katika mauzo na maonyesho ya tamthilia ya "Lovely Gamble" zitachangia watoto yatima na jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Uingereza.

0 comments:

Search This Blog