BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Wednesday, 19 May 2010

Viongozi wa Mgomo Nchini Thai Wajisalimisha

Vurugu kubwa zilizoleta maafa nchi Thailand zinategemea kuisha muda wowote baada ya viongozi wa mgomo huo kujisalimisha.

Watu wawili pamoja na mpiga picha kutoka nchini Italia wamepoteza maisha kutokana na vurugu za mgomo huo.

Raia wengine 17 wameumia akiwemo mwandishi wa habari kutoka Uholanzi ambaye aliyepigwa risasi ya mkononi. Pia mtengenezaji wa tamthilia kutoka nchini Marekani anatibiwa baada ya kupigwa risasi ya mguu.

Msemaji wa jeshi Colonel Sansern Kawekamnerd amesema wanajeshi wameingia kwenye maduka ya Rajpsong Shopping district, na waliweza kumiliki sehemu hiyo tangu mwanzoni mwa mwezi wa April.

Viongozi saba wa Red Shirt wameshindwa kuendelea na mgomo na kujisalimisha kwa selikali.

0 comments:

Search This Blog