BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday, 19 April 2011

ONGEZEKO LA SOKO LA NYAMA YA MBWA UCHINA


ONGEZEKO LA SOKO LA NYAMA YA MBWA UCHINA

WANAHARAKATI WANAJARIBU KUPINGA NA KUNUSURU MAISHA YA MBWA....
Labda kwa baadhi yetu tunachukulia mbwa ni mnyama anaefugwa kwa kuweza kusaidia katika maswala ya ulinzi au kuwa pambo fulani la kuipendezesha familia inayemfuga. Kwa wenzetu wa nchi za magharibi ya ulaya na Amerika mbwa ni mmoja ya (family membe)au Tuseme ni mwanachama wa familia ana haki sawa na wanandugu wengine waliomo katika familia! Pengine mbwa anathaminiwa zaidi kuliko wewe mgeni utakae tembelea familia hiyo.. Inawezekana kabisa mbwa akawa na chumba chake..lakini mgeni ukalala ukumbini. Nchini China kuna baadhi ya watu wanamtazamo tofouti kabisa juu ya MBWA..kuna baadhi ya wachina wanamchukulia mbwa ni sawa na wanyama wengine kama vile mbuzi,ng'ombe,kuku nk. kuwa mbwa anaweza kuchinjwa na kuliwa kama vile kitoweo kingine... Mtazamo huu wa baadhi ya wachina umeleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii ya wachina wapo wachina wanaopinga matumizi ya nyama ya mbwa na kuhakikisha kuwa mbwa anayo haki ya kuishi sio kuliwa.. Pia kuna wapo wachina wanaodai kuwa mbwa anafaa kuliwa na nyama yake inafaida fulani katika mwili wa mwanadamu..tena ongezeko la matumizi ya nyama ya mbwa nchini China limekuwa kubwa.. kiasi cha kutishia amani ya maisha ya mbwa katika nchi za ulaya na nyingine ambako mbwa wamekuwa wakiibiwa na kupelekwa sokoni uchina. Je?kweli kama kila mwanadamu ana hakai ya kula atakacho,hivi sisi wamatumbi tuna mtazamo gani ?juu ya hili la baadhi ya wachina? Baadhi yetu tumekuwa tukilalamikia matumizi ya mnuso wa nyama ya PANYA maarufu kama SAMAKI NCHANGA yanayotumiwa na baadhi ya watu hapa nchini,sasa kuhusu hili la washirika wetu wachina tunalitazamaje?
www.bongo-kwanza.com 

Sunday, 17 April 2011

MUHADHARA

BISMILLAHI RAHMANI RAHIIM


Tunawatangazia MUHADHARA utakaofanyika siku ya Jumaamosi, tarehe 23/04/2011 saa 10:30 jioni (16:30) Address KINGSHEATH COMMUNITY CENTRE, NORTH OVAL, NN5 7LN, NORTHAMPTON.

Mhadhara utatolewa na Sheikh Muhammad Eid (Abuu Eid) kutoka Tanzania. Tafadhari tuhudhurie. Kwa maelezo zaidi Tel: 07950635191 or 07919084078 Wabillah Taufiq

Wednesday, 6 April 2011

Fashion for London

Mji wa Aschaffenburg,Ujerumani kufungua msimu kwa AFRIKA FEST



Mji wa Aschaffenburg,Ujerumani kufungua msimu kwa AFRIKA FEST

Wakazi wa mji wa Aschaffenburg,nchini Ujerumani wanatarajia kufungua msimu wa siku za joto kwa sherehe za AFRIKA FEST, mjini Aschaffenburg,huko nchini ujerumani aka Ujeuri man.
Shamra shamra hizo za asiye na mwana abebe jiwe ,zinatarijiwa kuanza siku ya tarehe14 April hadi
16 April 2011,ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya sanaa,mziki na utamaduni kwa ujumla.
Na bendera ya Tanzania piga ua inawakilishwa na Dj maarufu "Mfundo pita"ambaye mwaka jana tu
alitajwa na redio mabali mbali nchini ujerumani kuwa ni DJ "Mkali wa midundo" ya World beat.
Mji wa Aschaffenburg,nchini Ujerumani mwaka huu 2011 ndio mji wa mwanzo kufungua dimba
la sherehe za msimu wa joto nchini humo,sherehe hizo zinatarajiwa kuudhuriwa na maelfu ya
wa watu kutoka kila kona ya ujerumani,

Mnakaribishwa wote..
kwa maelezo zaidi wasiliana simu +49(0)1733779720 au ndani ya ujerumani pia 01733779720

Search This Blog