Bank za kiIslam ni mipangilio
mbali mbali na tofauti tofauti ya kibenki kama vile kuhifadhi pesa, kuchukua
pesa, kusafirisha pesa kutoka bank kwenda bank nyengine na kutoka nchi moja
kwenda nchi nyengine , kufanya biashara kati ya mtu na mtu kwa msaada wa bank,
kufanya biashara kati ya mtu kwa kushirikiana na bank, kuuza bima za kiislam, kutoa mikopo kwa njia za
kiislam, Kuuza na kununua hisa kwa utaratibu wa kiislam na mengine mengi. Ni
vyema tukakumbushana kwamba bank za kiislam zinatoa huduma kwa waIslam,
wasiokua waIslam na hata wale wasiokua na dini yoyote.
Uhakika ni kwamba bank za kiislam zinakua kwa
kasi sana, bado kuna wataalam wachache ktk fani hiyo na hakuna sehemu nyingi ambazo watu wanaozungumza Kiswahili wanaweza
kupata maelezo mbalimbali kwa lugha yao, tumeona upo umuhimu wa kuanzisha blog
maalum ambayo wataweza kupata huduma hizo Kwa kutumia lugha tatu kiSwahili,
KiIngereza na kiArabu.
Ni muhimu kukumbushana kwamba
mafanikio ya uchumi wowote yanategemea uwiano kati ya maadili na mahitaji ya
binadamu, mshikamano wa vitu viwili hivyo ndio ambavyo vinajenga misingi ya
uchumi wa kiislam. Kuna wachumi wanaoona kwamba maadili ya uchumi wa kiIslam
yanawafanya washirika kugawana hasara na faida kitu ambacho kinasaidia sana
kuhamasisha kufanya biashara kwa maslahi ya jamii nzima.
Ukuaji wa bank za kiIslam
duniani wenye muelekeo wa kukataa riba ulioanza kujitokeza ktk kipindi takriban
cha miaka thalathini iliyopita, umetokana na muelekeo wa kimataifa wa
kuzikumbatia banki zinazokubali riba. Kwa mfano sifa kubwa ya mfumo wa uchumi
wa banki za kiMagharibi ulitegemea riba kwa kiasi kikubwa sana ambapo ilifikia
kiwango hata cha kupuuza dini zao. Kitendo hicho kilizidi kukua kwa kiasi
ambacho riba ilikua kama uti wa mgongo ktk uchumi wa Magharibi, kwa upande
mwingine uIslam uliendelea kung’ang’ania kwamba riba sio sahihi.
Inatosha kua (Judaism,
Christianity, Hinduism na Islam), zenye wafuasi zaidi ya theluthi mbili za watu
duniani zimeharamisha Riba. (For the Judaic and Christian views on interest see
Johns, et. al., and Noonan (1957) and for the Hindu view, see Bokare (1993), p.
168). Uislamu umeharamisha riba (2:278-279) Pia angalia Biblia, Deuteronomy 23:
19; Leviticus 25:36; Exodus 22:25; Ezekiel 18:5-9. Luke 2:34-35.
Inadaiwa kwamba presha
iliyotokana na mfumo wa bank za
kiMagharibi na ombwe lililokuwepo ktk uchumi wa kiIslam, viliwahamasisha wasomi
wa kiIslam kujaribu kuulezea uchumi wa kiislam ktk njia za kitaalam zaidi.
Wasomi wa kiislam ktk masuala ya kiuchumi waliamua kufuata misingi ambayo
ilikubalika ktk dini yao kama vile (Mudarabah), (Muraabaha) ambazo zina maana
ya kushirikiana, (Leasing) ambayo ina maana ya kukodisha na aina nyingine
nyingi za kiuchumi ambazo zinakubalika kiIslam.
Kwa maelezo zaidi: soma www.ijuebankyakiislam.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment