Wafanyabiasha
Wakitanzania washio jiji la London siku ya Jumamosi, tarehe 23, mwezi 2 walitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza Peter Kallaghe.
Lengo la ziara hiyo ni
kubadilishana nao mawazo na kuangalia jinsi gani wafanyabiashara hao wanavyoweza
kutumia fursa za kiuchumi zinazojitokeza nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo
wafanyabiashara hao walimueleza Balozi Kallaghe mafanikio yao na changamoto
zinazowakabili kwanye uendeshaji wa shughuli zao za kila siku.
Wafanyabiashara waliotembelewa
ni pamoja na Bi. Jennifer Wright anayemiliki biashara ya kuuza na kununua
nyumba pamoja na Soloon za nyele, Bw. Augustino Msey mwenye kampuni ya Swahili
Travel and Tours, Moona Store (dukani kwa Sadi) wauzaji wa vifaa vya umeme na
wakala wa Westen Union, Salumu wa Barking anayemiliki Foro Barbeque Food, na
pia Balozi Kallaghe alipata fursa ya kuhudhuria uzinduzi wa kikundi cha jamii
cha Istiqama UK. Balozi Kallaghe aliambatana na wanajumuia ya Kitanzania Bw.
Haruna Mbeyu na Bi. Mariamu Mungula.
Balozi Kallaghe alipokutana na
mmoja wa wafanyabiashara Bi. Jeniffer Wright alisema kuwa yupo tayari
kuwasaidia Watanzania waishio Uingereza na waliokuwepo nyumbani kwa kuwapa
mafundisho na maelekezo ya kibiashara kutokana na ujuzi aliokuwa nao. Pia Bi.
Wright aliomba serikali ya Tanzania ipunguze vizuizi vya biashara ili waweze
kuwekeza nchini Tanzania. Nae Mwenyekiti wa Swahili Group Bw. Augustino Msey
alisema kuwa kampuni yake inajitahidi kuitangaza Tanzania katika sekta ya
utalii. Bw. Msey aliendelea kusema kuwa kampuni yake inafanya mikakati mikunbwa
ya kuwekeza nchini Tanzania. Vilevile Forodhani Barbeque Food waliomba serikali
waliangalie suala zima la uraia pacha, kwani Watanzania wanapata tabu sana na
vizuizi vingi wanapotaka kuwekeza nchini.
Balozi Kallaghe aliwashauri
Watanzania wote wajumuike kwa pamoja, na washirikiane kuleta maendeleo na
kuwekeza nchini Tanzania na vilevile wanapopata matatizo wasisite kwenda
ubalozini kutaka ushauri na kuomba msaada.
Ally Muhdin - London
0 comments:
Post a Comment