www.bongo-kwanza.com
Tuesday, 19 April 2011
ONGEZEKO LA SOKO LA NYAMA YA MBWA UCHINA
WANAHARAKATI WANAJARIBU KUPINGA NA KUNUSURU MAISHA YA MBWA....
Labda kwa baadhi yetu tunachukulia mbwa ni mnyama anaefugwa kwa kuweza kusaidia katika maswala ya ulinzi au kuwa pambo fulani la kuipendezesha familia inayemfuga. Kwa wenzetu wa nchi za magharibi ya ulaya na Amerika mbwa ni mmoja ya (family membe)au Tuseme ni mwanachama wa familia ana haki sawa na wanandugu wengine waliomo katika familia! Pengine mbwa anathaminiwa zaidi kuliko wewe mgeni utakae tembelea familia hiyo.. Inawezekana kabisa mbwa akawa na chumba chake..lakini mgeni ukalala ukumbini. Nchini China kuna baadhi ya watu wanamtazamo tofouti kabisa juu ya MBWA..kuna baadhi ya wachina wanamchukulia mbwa ni sawa na wanyama wengine kama vile mbuzi,ng'ombe,kuku nk. kuwa mbwa anaweza kuchinjwa na kuliwa kama vile kitoweo kingine... Mtazamo huu wa baadhi ya wachina umeleta mtafaruku na mgawanyiko katika jamii ya wachina wapo wachina wanaopinga matumizi ya nyama ya mbwa na kuhakikisha kuwa mbwa anayo haki ya kuishi sio kuliwa.. Pia kuna wapo wachina wanaodai kuwa mbwa anafaa kuliwa na nyama yake inafaida fulani katika mwili wa mwanadamu..tena ongezeko la matumizi ya nyama ya mbwa nchini China limekuwa kubwa.. kiasi cha kutishia amani ya maisha ya mbwa katika nchi za ulaya na nyingine ambako mbwa wamekuwa wakiibiwa na kupelekwa sokoni uchina. Je?kweli kama kila mwanadamu ana hakai ya kula atakacho,hivi sisi wamatumbi tuna mtazamo gani ?juu ya hili la baadhi ya wachina? Baadhi yetu tumekuwa tukilalamikia matumizi ya mnuso wa nyama ya PANYA maarufu kama SAMAKI NCHANGA yanayotumiwa na baadhi ya watu hapa nchini,sasa kuhusu hili la washirika wetu wachina tunalitazamaje? Posted by Ally Muhdin at 01:16
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment