BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday, 11 April 2010

Al-HUDAA

Jumuiya ya Al-Hudaa ikishirikiana na New Deal Africa ambayo inaongozwa na Bw. Ayoub Mzee, walifanya sherehe za maulid ya mfungo sita katika ukumbi wa Wally Community Centre, jijini London nchini Uingereza. Maulid hayo yalikuwa kwaajili ya kumkumbuka Mtume Muhammad SWA aliyezaliwa mika 1400 AD iliyopita. Mtume Mohhammad amezaliwa Makka nchini Saudia Arabia, Baba yake ni Abdillah na mama yake Bi. Amina. Waumini na wageni waalikwa toka pande zote za dunia walihudhuria sherehe hizo. Maulid hayo yalijumuisha Dhikri, hotuba mbalimbali na Dua. Kwa taarifa zaidi tembelea www.ayoubmzee.blogspot.com na www.newdealafrica.com. Habari na picha Ally Muhdin

0 comments:

Search This Blog