BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday, 13 April 2010

Portsmouth kuomba kibali


nowyherb.png

Portsmouth wanafanya mpango wa kukiomba chama cha mpira nchini Uingereza kiballi cha kucheza kombe la barani ulaya.


Timu hiyo ambayo imeshuka daraja imeweza kujipatia nafasi ya kushirika katika kombe hilo baada ya kuweza kufika fainali za kombe la shirikisho la soka nchi Uingereza ambapo itapambana na Chelsea tarehe 15 May. Timu hiyo iliitoa Tottenham siku ya jumapili.


Portsmouth haitakiwi kushiriki mashindano hayo baada ya kushindwa kuomba kibali hicho, mwisho wa kuomba kibali hicho ulikuwa mwezi wa March 1.


Andrew Andronikou amesema kuwa kuweza kushiriki kwenye mashindano hayo kuleta changamoto kwa wanunuzi wanaotaka kununua timu hiyo. Watafanya kila njia kuweza kufanikisha mashindano hayo kufanyika Fratton Park. kushinda mechi yake


"Nafikiri ni muhimu kuweza kufikilia na kutumia njia zote za kuweza kucheza kombe la Ulaya" Andronikou alisema.


"Inajizungumza yenyewe, itakuwa bora zaidi na mafanikio makubwa kwa timu yetu na kuwavutia wanunuzi wa timu."


Kama watafanikiwa, Portsmouth watachukua nafasi katika ligi ya Ulaya kama washindi wa kikombe cha chama cha mpira nchi Uingereza FA na itaweza kuwaongezea kipato msimu ujao.


Wataki huohuo timu hiyo inataka kuzungumza na timu ya Lens yenye makazi yake nchini Ufaransa kuhusu mchezaji Dindane.


Aruna Dindane mkataba wake ni kuichezea Portsmouth mechi 21, siku ya nusu fainali ndiyo mechi yake ya 21, lakini kama ataendelea kuichezea timu hiyo mechi nyingine itawaghalimu Pompey malipo ya £4


Andronikou anauhakika watafakinikiwa maafikiano na timu hiyo ya Kifaransa.


Habari na Ally Muhdin, www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog