BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday, 13 April 2010

Carragher Awajibu wapenzi wa sokaJamie Carragher amejibu usemi wa wapenzi wengi wa mpira wa miguu ya kuwa Liverpool itapigwa na pengo kubwa itakapokosa kufaulu kucheza mashindano ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.


Timu hiyo inayotokea Anfield imeanza kukubaliana na matokea kama kuna uwezekano wa kushindwa kucheza kombe hilo la mabigwa wa ulaya ambolo wameweza kufanikiwa kucheza kombe hilo kwa muda wa miaka saba mfululizo.


Wekundu hao wanashikilia nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare na Fulham siku ya jumapili na wapo pointi sita nyuma ya Manchester City katika kugombea nafasi ya nne, vilevile wamecheza mechi zaidi.

beki huyo wa siku nyingi amesema haoni sababu yoyote kwanini wasiweze kurudi na kuwa na nguvu kubwa zaidi.


'Hakuna kitu kipya kama hatutofanilkiwa, kwani tumeshawahi kucheza na watu wanasahau hivyo' Alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.


'kama hatutofaulu msimu huu ninauhakika msimu ujao hautakuwa mbaya kama msimu huu'.


Carragher aliongezea kwa kusema: 'Tumeuanza msimu vibaya jambo ambalo hatukulitaraji. Tulipenda kushiriki kombe la mabingwa wa ulaya kuliko kombe la ulaya.


Kwa upande wangu kushinda vikombe ndiyo maana ya mashindano na ndiyo mchezo wenyewe, lakini kuna kushindwa pia katika mashindano.


Habari na Ally Muhdin, www.tz-one.blogspot.com0 comments:

Search This Blog