BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday, 13 April 2010

Adebayor ajiuzulu kuchezea timu ya TogoMshambuliaji maarufu wa timu ya Manchester City Emmanuel Adebayor ametangaza rasmi kujiuzulu kucheza mechi za kimataifa na kuichezea timu yake ya taifa ya Togo.

Adebayor amechukua uamuzi huo baada ya timu yake ya Togo kushambuliwa walipokuwa katika mashindano ya kombe la Africa nchini Angola.

Timu hiyo ya Togo ilishambuliwa na kusababisha watu watatu kupoteza kufariki.

Akitoa maelezo na sababu za kujiuzulu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema "Kutokana na tukio la shambulizi na ugaidi ambalo limesababisha watu wawili wa nchi mwake kupoteza maisha hiyo ndiyo sababu iliyomfanya kuchukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu kucheza mechi za kimataifa"


Akiendelea kutoa maelezo yake alisema kuwa "sisi ni wachezaji mpira tumeenda kucheza mpira na kuiwakilisha nchi yetu, lakini tumevamiwa na watu wanaotaka kupoteza maisha yetu, sitoweza kusahau na sihitaji kutokewa tena na kitendo hicho katika maisha yangu".


Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Cabinda nchini Angola. Magaidi waliivamia timu hiyo ya Togo na kuanza kurusha risasi. kitendo hicho kilisababisha mwalimu msaidizi na mwandishi wa timu ya Togo kupoteza maisha, pia dereve wa basi alipoteza maisha. vile vile beki wa timu hiyo Serge Akakpo na mlinda mlango Kodjovi Obilale kuumia. kundi la "The Front for the Liberation of the enclave of Cabinda" linashutumiwa kwa shambulio hilo lakini kundi hilo limekataa kuhusika na shambulio hilo.

Habari na Ally Muhdin, www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog