BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Thursday, 29 April 2010

Cheryl Cole Achaguliwa kuwa mrembo

Mwimbaji maarufu nchini Uingereza Cheryl Cole ameshika nafasi ya kwanza kati ya warembo maarufu mia moja wa FHM's duniani. Cheryl ameshikilia nafasi hiyo kwa mara ya pili mfululizo sasa.

Mcheza sinema Megan Fox pamoja na Marissa Miller walishindwa kuchukua nafasi hiyo yenye kugombewa na warembo wengi duniani.

Cheryl ambaye ameatengana na mumewe mchezaji wa timu ya Chelsea Ashley Cole, inasemekana kuwa mumewe alifanya mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine.

Ijapokuwa alipata matatizo katika ndoa yake lakini aliweza kushika nafasi hiyo ya kwanza na nafasi ya pili kushikiliwa na mcheza tamthilia ya Transformers Megan Fox na nafasi ya tatu kuchukuliwa na mwanamavazi maarufu ya Victoria Secret Merissa Miller.

Mchezaji wa tamthilia ya Twilight Kristen Stewart ameshikilia nafasi ya sita, Kelly Brook ambeye aliwahi kushika nafasi ya kwanza ametokea kuwa katika kumi bora.

0 comments:

Search This Blog