BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Thursday, 22 April 2010

Ryan Air Yakataa Kuwalipa Abiria


Ally Muhdin alipokuwa na Waziri wa mambo ya nje David Milliband.

Ryanair imekataa kuwalipa abria kutokana na matatizo ya usafiri wa anga uliosababishwa na mawingu ya moshi wa Volcano.
Meneja wa shirika la ndege la Ryanair MichaelO'Leary amesisitiza kuwa kampuni hiyo haitahusika na malipo yoyote yaliyosababishwa na mawingu ya moshi wa Volcano.


Ndege hiyo yenye kubana matumizi imesema kuwa haitalipa malipo ya nyumba za kulala wageni pamoja na gharama za chakula.


Bw. O'Leory amesema kuwa abiria wote watarudishiwa gharaza za tiketi na siyo gharama nyingine zozote.


Ryanair kwa siku inabeba abiria wasiopungua 220,000 wa nchi za Ulaya, Lakini Bw. O'Leary amesema hajui abiria wangapi wameathirika na matatizo hayo.


Waziri wa mambo ya Nje nchini Uingereza Bw. David Milliband amesema kuwa mashirika ya ndege yanabidi kuwapa abiria gharama za chakula na makazi ya kulala kwa wale walioathirika na maafa hayo.


Bw. Milliband amesema kuwa itakuwa si kitendo kizuri kama mashirika ya ndege hayatoa huduma hizo.


Wizara yake inajitahidi kuwasaidia raia wate walikumbwa na matatizo ya usafiri vilevile wanajitahidi kuhakikisha shule hazitotoa adhabu kwa wanafunzi wakakao kosa kufanya mitihani kutokana na matatizo ya usafiri.

0 comments:

Search This Blog