BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Saturday, 1 May 2010

Alikiba na TIDAlikiba na TID jana usiku waliwafurahisha wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jijini London, wanamuziki hayo walifanya tamasha katika ukumbi wa Club Afrique.

Wapenzi wengi walionyesha kufurahishwa na tamasha hilo lililowajumuisha wanamuziki hao wawili kwa pamoja.

Mwandishi wa Blog ya TZ-ONE Ally Muhdin alipomuhoji Christopher Chagula ambaye ni mpenzi wa muziki wa kizazi kipya kuhusiana na tamasha hilo alisema kuwa amefurahishwa na jinsi wanamuziki hao walivyoweza kufurahisha wapenzi wa muziki jijini London.

Wanamuziki hao watafanya onyesho lingine Reading siku ya jumapili katika ukumbi wa Face Club. Wanamuziki hao wamewahakikishia wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jijini Reading kuwa watafanya onyesho kabambe.

Mkurugenzi wa BongoDjs DJ Richie Richie amesema kuwa anawaomba wapenzi wa wanamuziki hao kufika mapema ili kuweza kufanikisha tamasha hilo.

0 comments:

Search This Blog