BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday 2 May 2010


Watanzania waishio nchini Uingereza walifanya sherehe za kusheherekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Kumuaga Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Mwanaidi Sinare Maajar ambaye amemaliza muda wake wa kazi nchini humo.

Sherehe hizo zilifanyika katika Ukumbi wa LA Royale Bonqueting Suites, Tottenham jijini London siku ya jumamosi.

Mgeni wa heshima Bi. Mwanaidi Maajar aliwashukuru watanzania kwa kuanzisha vyama na jumuiya ambazo zimewakutanisha na kudumisha umoja, upendo na kuwasaidia Watanzania waishio nyumbani na ughaibuni.

Balozi Maajar aliwahusia Watanzania kutokata tamaa katika kujishighulisha na kufanya biashara na kujiendeleza katika maisha yao kwani serikali ipo tayari kuwasaidia endapo wataonyesha moyo wa maendeleo.

"Nitapita kuwatembelea kuangalia maendeleo yenu yamefikia wapi" aliongezea Balozi Maajar ambaye amemaliza muda wake wa kikazi nchini Uingereza.

Naye Mwenyekiti wa chama cha Watanzania nchini Uingereza Bw. John Lusingo alitoa hutuba fupi ya kumuaga Bi. Maajar, "Tunakushukuru kwa kutuunganisha Watanzania na kutufanya kuwa kitu kimoja" Bw. Lusingo alisema.

Bw. Lusingo aliendelea kusema kuwa Balozi Maajar ametupa changamoto ya kuweza kuwa na umoja, uzalendo na imani katika mambo mbali mbali.

Jumuiya ya New Deal Africa ilitoa pongezi na shukrani kwa Balozi Maajar kwa mchango wake mkubwa wa kuiwezesha jumuiya hiyo kuweza kuanzishwa na kufikia hapo ilipo. Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya mwenyekiti wa New Deal Africa Bw. Ayoub Mzee, mwasisi wa Blog ya TZ-ONE Bw. Ally Muhdin alisema tusingeweza kuwa na mawazo ya kuanzisha jumuiya hii endapo tusingepata changamoto na ushauri kutoka kwa Balozi Maaajar.

Watanzania wengi walijitokeza katika sherehe hizo akiwemo mwimbaji maarufu wa Taarabu Bi. Sabaha Salum ambaye aliwatumbuiza washabiki wake kwa kuwaimbia nyimbo ya "FIMBO YA MUNGU"

African Band haikuwa nyuma illipata fursa ya kuwatumbuiza na kuwaburudisha Watanzania kwa kuwapigia nyimbo za kizamani ambazo zilitamba enzi hizo.



Ally Muhdin, London

1 comments:

Kitoto said...

Si viongozi wengi wanaosisitiza wananchi wapendane; iwe Bongo, iwe kimataifa. Tamko la namna hii litakuwa limetoka mdomoni mwa mwanamke. Baadhi ya wanawake madarakani huwa na kile wataalamu waitacho “inter personal skills” ambazo husaidia kuongoza kwa kuzingatia mawasiliano ya karibu zaidi na waongozwaji.
Chunguza.
Kati ya matatizo ambayo yamechangia wananchi kutoamini taasisi mbalimbali za kiserikali (ukiwemo ubalozi London) miaka iliyopita ni kuwa na viongozi wahuni, wasioaminika au bla bla, maneno matupu.
Katika muda mfupi Mama Maajar kajitahidi, kujaribu kuondoa usongo huu. Kati ya aliyofanya ni mathalan, kukutana na wananchi mara moja kwa mwezi, kusukuma vyama mbalimbali ikiwepo TAWA na mikutano miwili ya Diaspora London. Si ajabu alipigiwa makofi juzi. Na si ajabu wanawake wengi wakamwona kama mtu wa mfano (role model). Ila ile sherehe ilikuwa na tatizo la kukosa “ratiba” maalum. Hotuba nyingi, muziki kukatishwa katishwa, bendi kunyamazishwa na kutopiga zaidi miziki ya kwetu ya Kiswahili, nk.
Hili ni tatizo kubwa sana kwetu Watanzania. Kujifanyia mambo kiholela. Tutegemee siku zijazo udhaifu huo utarekebishwa maana Balozi keshapanda mbegu.

Search This Blog