BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday, 11 May 2010

Miliband Atabiriwa kuiongoza Labour Party


David Miliband amepewa nafasi kubwa ya kuweza kushika nafasi ya kuingoza Labour Party endapo Gordon Brown ataachia ngazi.

Bw. Miliband ambaye kwa hivi sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje yupo mstari wa mbele katika king'ang'aniro cha kugombea kukiongoza chama Labour Party.

Sehemu nyingi za kuchezea pata potea (Kamali) kama Paddy Power, William Hill na Ladbrokes zimetokea kumeweka katika nafasi ya juu ya kuweza kushinda.

William Hill wamesema watu zaidi ya 25 na kiasi kisichopungua paundi £1000 zimewekezwa kwaajili ya nani atakuwa kiongozi wa Labour Party.

Wengine katika king'ang'aniro hicho ni Waziri wa Elimu Bw. Ed Ball, Waziri wa Nishati Ed Miliband ambaye ni kaka David Miliband, Waziri wa Mambo ya Ndani Alan Johnson.

Miliband amezaliwa 15 mwezi wa saba mwaka 1965, Mbunge wa South Shields kupitia chama cha Labour Party tangu mwaka 2001.

Habari na Ally Muhdin

0 comments:

Search This Blog