BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Monday, 10 May 2010

Waziri Mkuu KujiuzuluWaziri Mkuu nchini Uingereza Mh. Gordon Brown atajiuluzu kuwa kiongozi wa Chama Cha Labour Party.

Mh. Brown's ametangaza uamuzi huo baada ya Chama chake kushindwa kupata kura za kuongoza nchi katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi.

Uchaguzi huo uliwafanya wananchi wa Uingereza kushindwa kuamua chama ambacho kitaweza kuwaongoza baada ya vyama vyote kushindwa kufikia viti 326 vinavyowezesha kuiongoza nchi.

Mh. Brown ataendelea kuingoza nchi na kuwa kiongozi wa chama hicho mpaka atakapopatikana kiongozi mwingine wa kukiongoza chama na Serikali.

Akizungumzia kuhusu masuala ya serikali ya nchi amesema kwamba shughuli zote za kiserikali zinaendelea kama kawaida.

Wakati huohuo chama cha Labour Party na Liberal Democrats vitakutana kujadili mwelekeo wa kuweza kuungana na kuunda serikali ya kuingoza nchi.


Ally Muhdin wa www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog