BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Friday 7 May 2010

Uchaguzi Wafanyika, Chama Tawala Hakijapatikana



Wananchi wa Uingereza jana tarehe 6 mwezi tano wamepiga kura kuchagua viongozi watakaoiongoza nchi kwa muda wa miaka mitano. Wananchi walianza kupiga kura tangu saa 07:00 Asubuhi mpaka saa 22:00 usiku.

Ijapokuwa kuna baadhi ya sehemu nyingine wananchi walishindwa kupiga kura kutokana na kuchelewa kufika katika sehemu za kupigia kura.Viti 650 ndiyo vilikuwa vinagombaniwa na mshndi wa viti vingi ndiye atakayeiweza kuongoza nchi.

Ili uweze kushinda inabidi upate viti 326 kuweza kuongoza nchi lakini vyama vyote vimeshindwa kufikia viti hivyo.

Matokeo ya uchaguzi yalianza kutangazwa kwa mshindi wa kiti cha Houghton & Sunderland baada ya Labour Party kushinda kiti hicho kwa kura 19137 kwa kupitia mgombea wao Bridget Philipson mwenye umri wa miaka 26. Mpaka kufikia mchana walimaliza kuhisabu kura katika majimbo yote ya uchaguzi.

Mpaka hivi sasa chama cha Conservative kinataka kuungana na Chama cha Lib Democrat Party ili kuweza kuongoza nchini.

Chama cha Conservative kimepata kura 305, Labour Party kura 258, Lib Democrat Party kura 57 na vyama vingine vimepata kura 28.

Uchaguzi umefanyika lakini hakuna chama chochote chenye nguvu ya kuongoza kutokana na kushindwa kufikia kiwango cha viti vya wabunge. Kwahiyo madaraka ya kuongoza yamebakia kwa Labour Party mpaka mshindi atakapopatikana.

Viti vya Wabunge vikifikia 326 ndivyo yinavyoweza kukipa chama nguvu ya kuweza kuongoza nchi na isiwe pungufu ya viti hivyo.

Ally Muhdin wa www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog