BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Saturday, 8 May 2010

Bingwa Ligi Kuu Uingereza Kujulikana Kesho

King'ang'aniro cha ubigwa wa ligi kuu nchini Uingereza kumalizika Jumapili, huku timu ya Manchester United na Chelsea zinagombea nafasi ya kuchukua ubingwa la ligi kuu.

Chelsea inaongoza kwa pointi moja na imebakiza mechi moja ya mwisho itakapopambana na Wigan siku ya Jumapili. Endapo Chelsea itashinda mechi hiyo basi itachukua ubingwa wa ligi kuu.

Wigan inayofundishwa na Roberto Martinez imeshawahi kuwafunga Chelsea kwa magoli 3-1, Arsenal 3-2 na Liverpool 1-0 katika michezo iliyochezwa uwanja wa DW ambapo zamani uwanja huo ulikuwa unaitwa JJB Sports.

kocha wa timu ya Wigan Roberto Martinez amesema kuwa mechi kati ya timu yake na Chelsea ni muhimu kutokana na kuwa ni mechi ya mwisho wa ligi na wapenzi wengi wa mpira wa miguu dunia watakuwa wanaangalia mechi hiyo kutaka kujua matokeo ambayo yataamuani kati ya timu ipi itachukua bingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, kwahiyo ni nafasi nyingine kwa timu yake kuonyesha mchezo mzuri na kuweza kushinda.

Manchester United ni mabingwa watetezi katika ligi kuu mpaka hivi sasa wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 82 na wamebakiza mechi moja na Stoke City siku ya Jumapili.

Mechi hiyo ni muhimu kwa timu ya Manchester United kushinda kwani bado wana nafasi ya kuchukua ubingwa endapo Chelsea watapoteza mechi yake wanayocheza na Wigan na hivyo basi Manchester United wataweza kuchukua ubingwa kwa mara ya 12.

Nafasi ya tatu katika ligi kuu inashikiliwa na Arsenal huku Tottenham imeweza kujichomeka katika nafasi ya nne ambayo ilikuwa inagombaniwa na Liverpool na Manchester City.

Tottenham Hotspur inashikilia nafasi ya nne baada ya kuweza kuwafunga Manchester City 1-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa City of Manchester. Goli pekee la Tottenham lilifungwa na Peter Crouch dakika nane kabla ya mpira kuisha.

Timu ya Tottenham yenye makazi yake jijini London imeweza kujipatia nafasi kuweza kucheza katika mechi za mabigwa wa Ulaya msimu Ujao.

Ally Muhdin wa www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog