BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Saturday, 8 May 2010

Wananchi waandamana Uingereza
Wanachama wa Liberal Democrats Party na wanachama wa vyama vingine walifanya maandamano kutaka kumuona kiongozi wa wa chama Liberal Democrats Party Nick Gregg.

Wananchi wengi nchi Uingereza wanataka chama hicho kifanye maamuzi yatakayo wanufaisha nchi na siyo yatakayo waletea matatizo. Moja ya maombi yao ni kuhusu upigaji kura katika uchaguzi ubadilishwe sabaubu watu wengi walishindwa kupiga kura na kuwanyima haki yao ya kuchagua viongozi watakaoweza kuwaongoza.

Watu wasiopungua 1000 walipiga makelele "Unatutumiaki Sisi", "Njoo Utusikilize" wakimaanisha tumekuchagua kutusikiliza matatizo yetu.

Mh. Clegg ambaye alikuwa katika ofisi za chama hicho akiongea na wabunge pamoja na viongozi wa chama cha Lib. Democrats Party, alitoka nje ya jengo la chama hicho na kusikiliza matakwa ya wananchi na kuwaambia kuwa ameingia kwenye siasa kwaajili ya kuunda na kurekebisha mfumo wa mzima wa siasa ya nchi.

Wakati huo huo chama cha Conservative kinachongozwa na David Cameron kimefanya mazungumzo na chama cha Lib. Democrats kuweza kuungana na kuunda serikali ya kuingoza nchi ya Uingereza.

Nae Mbunge kupitia chama cha Labour Party Bw. John Mann amemtaka kiongozi wa chama hicho Mh. Gordon Brown kujiuzulu nafasi ya Uwaziri mkuu.

Ally Muhdin wa www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog