BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday, 9 May 2010

Vyama vya Siasa Vyakutana


Vyama viwili vya siasa nchini Uingereza Liberal Democrats na Conservative Party vinakutana jijini London kujadili jinsi gani watavyoweza kuunda serikali ya pamoja ya kuingoza nchi.

David Cameron wa chama cha Conservatives, chama ambacho kimepata kura nyingi kushinda vyama vyote katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi lakini kimeshindwa kufikia idadi ya viti 326 vya kuweza kuingoza nchi, hivyo basi wanahitaji ushirikiano na chama cha Liberal Democrats kinachoongozwa na Nick Glegg kuweza kuunda serikali.

Vyama hivyo vitafanya mazungumzo leo 11 a.m Asubuhi, mazungumzo hayo yakikubaliwa na pande zote mbili yateweza kuindoa Labour Party madarakani.

Tayari mjadala wa maafikiano ushaanza na matokeo yake yatajulikana watakapomaliza mazungumzo.

Chama cha Labour Party walipoteza viti 91, Chama cha Liberal Democrats Party walipoteza viti 5, Chama cha Conservative Party waliweza kujiongezea viti 97, vyama vingine walipoteza kiti kimoja na Chama cha Green Party kilweza kushinda kiti kimoja kwa mara ya kwanza katika uchaguzi huo.

Chama cha Labour Party kinasubiri kama vyama hivyo vitakaposhindwa kuafikiana ili kuweza kuungana na Liberal Democrats Party kuunda serikali.

Ally Muhdin wa www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog