BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday 4 May 2010

Viongozi wa TA Wasimikwa Reading




Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza kiliwakabidhi rasmi madaraka viongozi wa chama hicho katika ukumbi wa The Warehouse jijini Reading.

Viongozi wa jumuiya ya TA walichaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa nne jijini London, Uingereza.

Jumuiya hiyo iliwaalika viongozi mbalimbali wa kitaifa na vyama visivyo vya kiserikali kuhudhulia halfa hiyo, mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Mwanaidi Maajar.

Katika sherehe za Jumiya hiyo huko Reading, Mh. Balozi aliandamana na Mh. Wilson Masilingi , Mbunge wa Muleba Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya inje na Ulinzi, Mh. Masilingi aliambatana na Mh. Hassan Zungu, Mbunge wa Ilala , lakini pia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mambo ya nje na Ulinzi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza, Dr John Lusingu, alianza kwa kumshukuru Mh. Balozi Maajar kwa kudumisha umoja na ushirikiano ambao umetokea kupendwa Uingereza, vilevile kusaidia jumuiya pamoja na Watanzania kwa kuwakutanisha na viongozi wa serikali na vyama toka nyumbani Tanzania wanapofika hapa Uingereza katika ziara zao, kuanzia Raisi Jakaya Kikwete, Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Wazari Membe na viongozi wengine wa kiserekali.

Mwenyekiti, pia alitumia fursa ya ugeni huo kuikumbusha serikali kwa kupitia waheshimiwa hao kwamba Jumuiya ya Watanzania ilyopo hivi sasa ni tofauti sana na zile za miaka iliopita, kwani kwa sasa wana umoja, upendo, na ushirikiano wa hali ya juu na sasa wako tayari kuliko siku zote kushiriki kikamilifu katika kuchangia ujenzi wa Taifa kwa kupitia huduma zao, mawazo yao, kwa hali na mali.

Dr. Lusingo aliowaomba viongozi wengine wa serikali kuipa msingi imara njozi ya Raisi kuhusu diaspora ili isiishie katika majukwaa bali kuwe na tofauti zinazotambulika kutokana na mchango wa watanzania ughaibuni wingereza.

Kabla ya kuanza hotuba yake Mh. Balozi, aliwaalika Mh. Zungu kuamukia Watanzania, Mh. Zungu alifurahi sana kuwa katika shuguli ya Kitanzania katika ukumbi uliofurika, na kupendezshwa na rangi za bendera ya taifa la Tanzania, aliwakumbusha Watanzania, kufanya kila linalowezekana kuwa na nguvu ya pamoja kuliendeleza taifa lao na kudumisha yale mambo ambayo Balozi Majaar ameyaanzisha, naye Mh Masilingi aliwafurahisha Watanzania, pale alipowaambia kuaw hata kama kunasababu zilizowafanya baadhi yao kutafuta uraia wa nchi zingine, utaifa wao bado ni hazina kubwa na wasijivunie utaifa wao wanaopokuja nyumbani kwani ndio kwao na hakuna Mtanzania alie na muda wa kuchunguza mambo yanayohusu uraia wao wa nchi nyingi kama hauhatarishi usaalama wa Taifa. Kuhusu hoja ya Uraia pacha . Mh.Masilingi alikiri kuoongolewa baada ya kuwa na mjadala kidogo kuhusu swala hilo na baadhi ya waTanzania, isipokuwa alioonya kuwa ni vema mawazo toka pande zote za Mjaadala yapokelewe kwa makini.

Naye Balozi Maajar, alimshukuru M/K kwa mchanganuo wake kuhusiana na jinsi Jumuiya ilivyobadilika katika muda wake hapa Uingereza, Mama Maajar huku akikatizwa mara kwa mara katika hotuba ya na wimbo Mama, Mama, Mamaa, Mama Huyo !ambao umejitokeza kuwa maarufu kama ishara ya kuuafiki umahiri wa uongozi wake na mapenzi ya Watanzania Uingereza, aliendelea kuawkumbusha Watanzania huko Reading kuwa yote yaliwezekana kwa sababu ya ushirikiano wao, aliwaomba Watanzania waendeleze mshikamano huo na ubalozi na hata atakokuja balozi mwingine. Mh. Maajar aliwashukuru Mh. Masilingi na Mh. Zungu kwa kukubali kwao kujumuika na Watanzanai Reading licha ya uchovu wa safari kwani walifika asubuhi ya jumatatu.

Baadaye Mh Balozi Maaja aliongoza mnada wa kuchangia mfuko wa Jumuiya hiyo Reading hii ilikuwa baada ya shuguli hiyo kusuasua. Balozi alifanikiwa kuchangisha kiasi cha fedha kisichopungua paund £300 za kingereza, na dola $50 za Kimarekani kutoka kwenye leso ya kimaasai ya pauni £20. Katika hafla hiyo Mdau wa Urban Pulse aliahidi kuwa siku ya uzinduzi wa tamthilia ya Lovely Gamble, atachangia asilimia tano ya mapato kwa Jumuiya Watanzania Reading. Naye Sporah show alichangia pauni £5o , Mh. Zungu Dola $100, na Mh.Masilingi Pauni $50.

Mwandishi wetu Ally Muhdin wa Blog ya TZ-ONE alipowahoji wanachama wa jumuiya hiyo walisema wafurahishwa na mchango mkubwa alioutoa Balozi Maajar katika kufanikisha sherehe hizo na kuweza kuwaletea viongozi wa Kiserikali kuja kujumuika nao.

0 comments:

Search This Blog