BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Friday, 14 May 2010

Warembo wakataa Kuvaa Bikini


Pichani Miss England, Lance Corporal Katrina Hodge katikati akiwa na Miss London finalists, Kimberley Cooper kushoto na Anna Watts kulia


Warembo watakaoshikiri mashindano ya kumtafuta mshindi wa Miss London mwaka huu kutovaa nguo za kuogelea, badala yake watavaa mavazi ya michezo.

Tangu miaka 60 iliyopita washiriki wa mashindano hayo walikuwa wanavaa nguo za kuogelea.

Mawazo mazuri ya kutovaa nguo hizo yalitolewa na mshindi wa mwaka jana 2009 Katrina Hodge pamoja na washiriki wengine.

Katrina mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa "Katika masuala ya urembo siyo vizuri wanawake kuonyesha wembamba uliopita kiasi"

Aliendelea kwa kusema kuwa wanataka kuonyesha kuwa mwanamke wa Kiingereza ni zaidi ya mwanamke wa kweli na mwenye kujiheshimu.

Hawapendelei wakionekana kwenye magazeti na watu kuwasema "Eh Mungu, Mwangalie huyu mwanamke" wakati ukweli ni kwamba wanapokuona kwenye picha na jinsi ulivyo tofauti.

"Nimeshiriki mashindano ya Miss England mara mbili mfululizo nimekutana na wanawake wakijinyima kula na kuogopa kuhusu kuvaa bikini na mimi naona siyo mtazamo mzuri kwa wanawake, hivyo basi iondolewe"

Mavazi ya michezo watakayovaa katika mashindano yamedhaminiwa na Kings Road Sporting Club.

Ally Muhdin www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog