BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Thursday, 13 May 2010

Serikali Mpya Yajipunguzia Mishahara.Serikali mpya ya Uingereza inayoongozwa na Mh. David Cameron imejipunguzia mishahara kwa asilimia 5% kwaajili ya kupunguza bajeti ya rekodi ya madeni.

Vyama vya Conservatives na Liberal Democrats Vimekubaliana siku ya Jumanne kuweza kushirikiana katika kupunguza madeni yanayoikabili nchi na pia kupambana na hali ngumu ya uchumi wa nchi.

Baraza zima la Mawaziri limekutana siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza kujadiliana mikakati ya kuendesha nchi na kujipunguzia mishahara.

Waziri Mkuu David Cameron mshahara wake utapungua toka Paundi £150,000 mpaka kufikia Paundi £142,000 na viongozi wa chini yake watapokea Paundi zisizozidi £135,000 kwa mwaka.

Mawaziri wote watapunguziwa mishahara yao kwa muda wa miaka 5. Kitendo hicho kitasaidia kuokoa kiasi cha Paundi millioni tatu za Kiingereza.

Habari na Ally Muhdin www.tz-one.blogspot.com

0 comments:

Search This Blog