BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Saturday, 12 June 2010

CHAMA CHA MAPINDUZI

TAWI LA UNITED KINGDOM
Ombi la Chama Kuchangia Uchaguzi Mkuu wa CCM Oktoba 2010


Ndugu Mzalendo,


Kwa heshima na taadhima ya dhati tunayo furaha ya kukuarifu kuwa, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewaomba wanachama wote wa CCM na
wasio kuwa wanachama lakini wenye mapenzi mema na Tanzania ,kukichangia chama katika uchaguzi mkuu ujao baadae Oktoba mwaka huu.


Halmashauri kuu ya CCM United Kingdom katika kikao chake cha Mei -1- 2010, kiliunda kamati maalum ya kusimamia na kutekeleza ombi la agizo hilo.


Kwa hivyo basi ,kwa uzalendo wako kwa taifa lako Tanzania na watu wake,tunaomba mchango wako kwa kiasi chochote utakachojaliwa nacho na tunakuahidi kuwa mchango wako utawasilishwa moja kwa moja Makao makuu ya Chama Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa chama ambapo viongozi wakuu wa CCM United Kingdom watahudhuria na kuwasilisha mchango wako huko.


Shime wana Ndugu, Mzalendo tushikamane katika kutekeleza ombi hilo la Mwenyekiti wa chama taifa kizalendo ili tuonyeshe kuwa kweli tupo imara kutoa mchango kwa taifa letu.Tunaomba mchango wako uwe umeifikia kamati kabla ya mwisho wa mwezi wa sita, ili michango yote ya wapenda CCM iwasilishwe Dodoma katikati ya mwezi Julai.


Unaweza kuwasilisha mchango wako moja kwa moja katika Akaunti ya CCM UK ambayo ni;

Benki: Lloyds TSB (UK)

Branch: Market Place, Reading

Jina la Akaunti: Chama Cha Mapinduzi

Akaunti Namba: 0587300

Sort Code: 30-96-96;

IBAN NUMBER: GB75 LOYD 309696 9600 5873 00


*Tafadhali andika jina lako kama reference ili tuweze kukuandika katika orodha ya watu waliojitolea ambayo itapelekwa Makao Makuu Dodoma.


“MTU KWAO:Watanzania tuna jukumu la kuijenga Tanzania popote pale tulipo”


Imetolewa na Wanakamati;


Hassan Hafidh – Mwenyekiti wa Kamati - 07536497772
Lilian Barongo - 07525175337
Mariam Mungula - 07770910901


Tunatanguliza Shukrani za dhati.0 comments:

Search This Blog