BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Tuesday 8 June 2010


WAZIRI KUKUTANA NA WATANZANIA UK

Waziri wa Afrika Mashariki Dr. Deodoras Kamara anategemewa kufanya ziara ya siku tatu kuzungumza na wanajumuiya wa hapa Uingereza. Ziara hii ni kwa ajili ya kuchambua na kupata mawazo mbalimbali kutoka kwa watanzania waishio Uingereza kuhusu maswala ya Afrika Mashariki (uhamiaji, soko huria, umuliki wa ardhi, biashara, n.k). Ziara hii inafuatia ahadi aliyoitoa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alipoitembelea jumuiya hivi karibuni.


Tanzania Association taifa ambayo inasimamia swala hili ikisaidiwa na ubalozi, imeyatambua maeneo matatu ambayo Dr Kamara atayatembelea na tarehe na muda kama ifuatavyo:

Tarehe

Mahali

Muda

Kuanzia Hadi

18-06-10

London

10:00

12:00

19-06-10

Reading

09:00

11:00

20-06-10

Manchester

07:00

09:00


Inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Luton, Oxford, Milton Keynes, Slough, Bristol, Birmingham, Coventry, Northampton na maeneo mengine ya karibu watahudhuria kongamano la London au Reading.

Vile vile inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Leicester, Leeds, Liverpool na maeneo mengine ya kaskazini mwa UK watahudhuria kongamano la Manchester.

Hata hivyo, hakuna kinachomzuia mwananchi kuhudhuria kongamano lolote kati ya hayo hapo juu iwapo tu atatimiza sharti moja kama ilivyoorodheshwa hapo chini.

Angalizo: Ili kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata nafasi ya kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika hali ya usalama na isiyo na usumbufu, wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika mkoa ambapo kongamano wanalotegemea kuhudhuria litafanyika.

Utaratibu wa kujiandikisha kwa mkoa wa London tumia e-mail ifuatayo: HYPERLINK "mailto:talondon@gmail.com" talondon@gmail.com

Kongamano la London litafanyika ubalozini:

Tanzania High Commission

3 Stratford Place W1C 1AS, London.

Kwa maeneo mengine, TA taifa itatoa maelezo zaidi hivi karibuni.

Kwa wananchi Reading, kongamano litafuatiwa na sherehe maalumu - Tanzania Night. Kwa maelezo zaidi tafadhali fuatilia habari hii.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ziara hii tafadhali wasiliana na TA taifa hapa:

HYPERLINK "mailto:watanzaniauk@hotmail.co.uk" watanzaniauk@hotmail.co.uk

07846783365 or 07536497772

KWA NIABA YA UBALOZI NA TA WOTE MNAKARIBISHWA

By Director of Communication - TA National


0 comments:

Search This Blog