BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Wednesday, 25 August 2010

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Agosti 27 mwaka huu, inatarajia kutoa uamuzi endapo mshtakiwa namba moja katika kesi ya kuomba rushwa ya h milioni 10, mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Taifa (TBC1), Jerry Murro, na wenzake, kuwa na kesi ya kujibu ama kuachiwa huru.
Uamuzi huo umefikiwa jana baada ya upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi juu ya watuhumiwa hao katika kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Gabrile Milumbe alidai ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka umekamilika hivyo mahakama imefunga na inatarajia kutoa uamuzi huo endapo watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu au la.

‘Tunafunga ushahidi na Agosti 27 mahakama itatoa uamuzi juu ya kesi hii ili kufahamu kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu au kuachiwa huru,” alidai Hakimu Milunde.

Awali mtuhumiwa namba tatu, Deogratius Mugassa, alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa alilazimishwa kukubali na kusaini maelezo ya kituo cha polisi ili kumkandamiza mtangazaji huyo.

Mtuhumiwa huyo alisema awali hakumfahamu mtangazaji huyo, zaidi ya kumuona kwenye runinga, ambapo akiwa Kituo cha Polisi cha Kati na Makao Makuu ya Polisi alipewa maelezo na kushinikizwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZDCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo, na Kamishna Kasala kuwa anamfahamu ili mshtakiwa wa kwanza (Murro) awe na kesi ya kujibu.

Katika maelezo yake, Mugassa alidai Jeshi la Polisi lilikuwa likimsaka kwa muda mrefu mtangazaji huyo kutokana na kusababisha kifo cha askari wao na wengine kufukuzwa kazi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Gabrile Milumbe, Mugassa alisema hata hati ya maelezo iliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali Stanislaus Boniface, sio ya kwake na haina ukweli wowote.

“Nakumbuka Februali 3 mwaka huu, wakati tukiwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam, ZDCO Mkumbo akiwa na maofisa wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), pamoja na askari wengine nilipewa maelezo ambayo tayari yameshaandikwa na kulazimishwa kusaini ili kuonekana ni ya kwangu, wakati sio kweli,” alisema mtuhumiwa Mugassa.

Akipinga hoja za mtuhumiwa huyo, wakili wa serikali, Stanslaus Boniface, alidai ni jambo la kushangaza kwa mtuhumiwa kusaini kitu ambacho hakifahamu.

Wakili: Hebu soma kifungu cha hapo chini…., ni sahihi ya nani?

Mtuhumiwa: Ni ya kwangu, lakini nililazimishwa kufanya hivyo.

Wakili: Fungua hapo mbele halafu soma, na ielezeee mahakama ni saini ya nani?

Mtuhumiwa: Ni ya kwangu kweli, lakini nimeshaeleza nililazimishwa kufanya hivyo kwa ajili ya kumkandamiza Jerry Muro.

Februali mwaka huu, Murro, Edmund Kapama na Muggasa walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa ya kushawishi na kuomba rushwa toka kwa mhasibu wa Halmashauri ya Bagamayo, Michael Wage.

Posted by Stanley Kadilana.

0 comments:

Search This Blog