BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday, 1 August 2010

PONGEZI
Zanzibar For Democracy inachukua nafasi hii kuwapongeza wazanzibari kwa uamuzi wa kihistoria waliouchukua kwa kupiga kura ya NDIYO katika zoezi la kura ya maoni. Sisi tunaamini kuwa uamuzi huo utafungua ukarasa mpya wa maendeleo na kuipeleka Zanzibar katika Demokrasia ya kweli ambapo wananchi wenyewe watakuwa ndio watakaokuwa na mamlaka, madaraka na uamuzi wa mwisho kuhusu mambo yote ya nchi yao.

Ushindi huo wa kura ya NDIYO unaweka bayana kuwa wananchi wamekubali kujenga jamii mpya yenye kuthamini utu wa mtu na ubinadamu na kuhakikisha kuwa Zanzibar itaongozwa kwa sera zenye kufuata misingi ya uhuru,haki, udugu na amani yenye kudumisha SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ambayo itakuwa ni kichocheo katika nyanja zote za maendeleo na utamaduni wa Visiwa Vyetu na watu wake.
Ahsante,
UONGOZI,
ZANZIBAR For Democracy,
LONDON,

0 comments:

Search This Blog