BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Wednesday, 26 October 2011

KHADIJA KOPA UK TOUR
Malkia wa mipasho Bi. Khadija Kopa ameingia leo jijini London akitokea Dar Es Salaam tayari kwaajili ya onyesho lake litakalofanyika Milton Keynes siku ya Jumamosi 29th October 2011 katika ukumbi wa The Golden Lounge, Unit 35 Baton Rd, Milton Keynes, MK2 3LH.

Akizungumza na mwadishi wa blog ya TZ-ONE ya UK Bw. Ally Muhdin, Malkia wa mipasho aliwaahidi wapenzi wake kuwa atawafurahisha na kuhakikisha wataburudika na nyimbo zake mpya na zile za zamani.

Vilevile kampuni ya African Splash promotions pamoja na Infinity Entertainment wamewaomba wapenzi wote wa Khadija Kopa kujitokeza kwa wingi kwenye ukumbi wa The Golden Lounge, Milton Keynes kwaajili ya kuweza kumuona mwanamuziki huyo.

0 comments:

Search This Blog