Katika Gazeti la Mwananchi la tarehe 16/5/2012 kulikuwa na makala iliyonakili ushauri wa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Kayanza Pinda akizishauri bank zitoe mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima. Alizitaja changamoto ambazo zinawakabili wakulima kwa kusema ‘"Wakulima wadogowadogo wanashindwa kupata mikopo ya kutosha kwa sababu benki za biashara zinawatoza riba kubwa na kuhitaji dhamana (collateral) alisema Mh Pinda.
Mh Pinda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Kilimo Vijijini Afrika (Afraca).
Malengo hasa ya kuandika makala hii ni kujaribu kuishauri serikali na wananchi kwa aujumla jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo kwa kutumia taasisi nyingine za fedha kama vile bank za kiIslam. Kwa upande mwingine tunapenda kuzishauri bank za kiIslam kuanza kufikria uwezekano wa kutoa huduma hizo kama bado kwa sasa hazipo.
Tukianzia na tataizo la riba (interest), ni dhahiri kua riba ktk mazingira yake yote ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Matatizo ya riba yalishaelezwa na bado yanaendelea kuelezewa, na kuthibitishwa na wataalam wengi wa kiuchumi duniani, kwa mfano hivi karibuni mkuu wa shirika la fedha la kimataifa International Monetary Fund (IMF) Christine Lagarde aliishauri serikali ya Uingereza kupunguza kiwango cha riba mpaka ifikie sifuri, alinukuliwa akisema “BRITAIN should consider cutting the interest rate to ZERO if the economy continues to struggle, the International Monetary Fund believes”). The Sun 23 may 2012. Maneno ya Miss Lagarde yaliungwa mkono na wanauchumi wengi kwa kesema “Cutting rates from 0.5 per cent won’t be the solution on its own, but would send out the right signal.”
Kwa upande wa bank za kiIslam, tungezishauri zijitokeze kuwafahamisha wananchi na wadau mbali mbali kua ziko njia mbali mbali zinazoweza kutumiwa kuepuka riba, na wakati huo huo kuleta ufanisi katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, jamii na kadhalika. Ukweli ni kwamba bank za kiIslam zina uwezo wa kuwasaidia wakulima kwa kutumia mifumo ya uchumi ambayo inakubalika kisheria kama vile murabaha, mudarabah, muzaarah, musaqaat na nyinginezo ambazo zimeelezewa kwa ufasaha kwenye www.ijuebankiyakiislam@blogspot.com.
Tukitolea mfano kwa kutumia mfumo wa murabaha, bank inaweza kuwapatia wakulima vifaa na mahitaji mbali mbali kwa masharti ya kulipa hapo baadae pamoja na faida. Murabaha maana yake ni bank au mwenye uwezo, kumnunulia asie na uwezo kitu fulani kwa masharti amlipe kwa faida maalum hapo baadae, kwa mfano bank inaweza kuwanunulia wakulima vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrector, mbegu na mbolea, kisha ikawauzia kwa faida maalum kwa masharti walipe hapo baadae. hapa inaonekana wazi kabisa kua murabaha unaweza kuwasaidia wakulima wakaweza kujikomboa na kujitegemea hapo baadae.
Wasi wasi mwengine ni ule unaohusiana na dhamana (collateral) kutoka kwa wakulima kutokana na uhakika kwamba wakulima wengi hawana mali ambazo wanaweza kuzitumia kama dhamana ili bank ziweze kuwapa mikopo. Hilo nalo linaufumbuzi wake, kwa mfano bank za kiislsm inaweza ikatumia kitu kinachojuikana kama ‘group-based lending approach capitalising on peer monitoring and guarantee mechanism’ ambayo ni utaratibu wa kufanya biashara kwa vikundi ambayo hiyo inaweza kuwa mbadala wa dhamana kwa mtu mmoja mmoja.
Ushauri kwa serikali ya Tanzania
Kwa upande wa serikali, tunapenda kuishauri ibadilishe njia (approach) katika kilimo na wakulima kwa kuweka mipango madhubuti ya mabaliko katika maeneo mengi ya vijijini kwa kujenga miundominu. Ni ukweli usiopingika kua wakazi wengi wa vijijini wanapoteza haki zao za msingi kama vile elimu bora, matibabu ya uhakika, na kadhalika. Ukiangalia umuhimu na mchango wa mkulima katika mataifa yanayoendelea utakuta kwamba wakazi hawa wanatakiwa wapatiwe mahitaji muhimu kama vile barabara safi, vituo vya elimu, afya na miondombinu mengine. Kwa kua wakazi wengi wa vijijini ni wakulima, serikali pia inatakiwa iweke mipango madhubuti ya kuinua kilimo kwa kuwapatia wakazi hawa wataalam,ujuzi na mahitaji mengine.
Pamoja na mambo mengine hotuba yake Mh waziri mkuu iliziasa bank kuwafikia wananchi huko vijijini, hili ni suala muhimu kwani mabank mengi yamejikita sana mijini na kuwasahau kwa kiasi kikubwa wakazi wa vijijini. Wataalamu wengi wa kiuchumi wanadai kwamba suala la faida kwa mabank ndio sababu ya mabank haya kutokupeleka huduma vijijini, suala hili limesababisha wakazi wengi wa vijijini kukosa huduma za kibank mpaka waende mijini kitu ambacho kinawagharimu sana. Kwa upande mwengine uchunguzi wa mambo unaonyesha kua wakazi wengi wa vijijini hawana bank accounts, kitu ambacho kimesababisha ugumu sana kwa wakazi hao kuaminika kupata hata hiyo mikopo yenye riba nafuu.
Maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasaidia wakulima na kupambana na changamoto zilizopo yataelezewa kwa ufasaha na kila moja itatengewa sehemu maalum kwenye www.ijuebankiyakiislam.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment