BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday, 8 July 2012

Riba (interest) ya LIBOR yaiweka pabaya Barclays bank


London Interbank Offered Rate (LIBOR) ni makadirio ya kiwango cha riba kinachotumika wakati benki zinapokopeshana pesa. Kiwango hicho cha riba kinatumiwa na mabenki yanapokopeshana kwa kulipa mikopo ya muda mfupi na muda mrefu (siku moja, mwezi hadi mwaka) Kiwango hicho kinawekwa na British Bankers’ Association (BBA) kila siku saa tano asubuhi kwa time za Uingereza. 
Taasisi za pesa wanapotoa mikopo, credit card au (Mortgage) kumkopesha mteja nyumba, wanawatoza wateja kiwango cha riba kulingana na kile kiwango cha riba kilicho pangwa na BBA (LIBOR) au wanaongeza zaidi. LIBOR kwa kawaida inatumika kama kigezo (benchmark) cha kiwango cha riba kwa pound ya kiingereza na sarafu za nchi nyingine nyingi. Kinachofanyika ni kwamba kila siku, benki 16 zinatakiwa zitaje kwa wawakilishi wa mabenk (BBA) kiwango cha riba (borrowing cost) kinachotozana pindi mabenki hayo yanapo kopeshana.
LIBOR imezusha mjadala mkubwa  kuhusu uhalali wake na vigezo inavyovitumia ktk kufanya kazi kwake, kwa mfano gavana wa bank ya England  Mervyn King ameripotiwa akisema ‘wakati umefika kwa LIBOR kubadilsha utendaji wake wa kazi kutoka kwenye makadirio na kwenda kwenye kuangalia jinsi soko la biashara lilivyo ili kujua vipi riba inaweza kukadiriwa. 
Moja ktk vitu ambavyo vimekua na mshituko mkubwa kuhusiana na utumiaji wa Libor ni pamoja na ile ya kutozwa faini ya pound 290 million Barclays bank kwa kile kilichodaiwa kwamba kwa makusudi wameweka kiwango maalum cha LIBOR (kufix) kwa maslahi ya bank hiyo. Kwa mujibu wa taarifa rasmi mbalimbali ambazo zilizoandaliwa Marekani na uingereza zimeeleza kwamba, kulikua na mazungumzo kati ya viongozi wa juu wa Barclays na viongozi wa mabank mengine ambapo ilidawa kua bank nyingine zilionyesha wasiwasi wao kutokana na kiwango cha riba cha Barclays kua juu ukilinganishe na kile cha bank nyingine. 
Kufuatia maelezo hayo tumeona ipo haja ya kulizungumzia swala zima la LIBOR kwa ujumla na uhusiano wa LIBOR na bank za kiislam kwa ufupi. Tukirudi kwa upande wa bank za kiIslam, wasomi wengi wameonyesha waiwasi wa kutumia LIBOR kwa sababu kuna mazingira ya riba ambayo hayakubaliki kisheria. Pamoja na mambo mengine, mwaka 2011 Islamic bank ilifanikiwa kupata the Islamic Interbank Benchmark Rate (IIBR). Kwa ufupi, IIBR ni kiwango cha faida ambacho kinakubalika na Mabank kwamba kimekamilisha masharti yanayokubalika na sheria ya kiIslam, Mabank yanafanya hivyo kwa kukubali kutoa na kupokea kiwango hicho kulingana na hali halisi ya soko la biashara. Makadirio ya kiwango hicho yanafanyika kabla kidogo ya saa tano asubuhi kwa taimu za Makkah ambayo ni sawa na taimu za (GMT + 3).
 Kinachotokea ni kwamba kinanyakuliwa kiwango cha Mabank 16 na Thomson Reuter saa 10. 45 AM kila siku kuanzia Jumapili mpaka Al khamis. Bank zinaombwa zitaje kiwango chao kati ya saa 9.00 AM- 10.44 AM kwa taimu za Makkah ,na zinatakiwa zijibu maswali yafuatayo. Ni kiasi gani cha faida  yatapenda kushiriki kwa ajili ya inter-bank ambayo inafuata sheria ya kiislam na je yatakubali kuuza na kununua kwa kiwango hicho kwa muda wa siku moja au wiki moja na kuendelea. Baada ya hatua hiyo, Thomson Reuters inajiridhisha kwamba utaratibu umefuatwa kwa kufanya audit na kwa kuhakikisha kwamba kiwango kilichotajwa ni sahihi na wanachukua wastan utakaopatikana ktk Mabank hayo 16 na kiwango hicho kinatumiwa kupatikana IIBR. Tofauti nyingine ni ile ya sheria ya kiislam kuzuia kamari (speculation) na hadaa (gharar), na kuzuia biashara ambazo sio halali kisheria. Faida ya mtaji ktk uchumi wa kiIslam inategemea jinsi gani mjasirimali atakua tayari kukubali hasara inayotokana na biashara na sio kutegemea riba. Upande mwingine ni ule unaohusiana na kuuza deni pamoja na kutaka uhakika (guarantee)  ya faida, hilo haliruhusiwi ktk sheria ya kiIslam na badala yake mifumo mingine ya kibiashara inaweza kutumika kama vile Mudarabah na musharakah.
Kufuatia scandal ya LIBOR bado inaendelea na kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua muelekeo mwengine kabisa ktk wakati wa baadae lakin hadi sasa, mwenyekiti   wa Barclays Marcus amejiunzulu Jumatatu ya tarehehe 2/07/2012 na mkurugenzi (Chief executive) wa Barclays Bob diamond nae amejiunzulu kufuatia shinikizo la wanasiasa. Kwa maelezo zaidi na ushahidi wa hayo soma www.ijuebankyakiislam@blogspot.com 

0 comments:

Search This Blog