Waziri wa Nishati na Madini Mh. Sospeter
Muhongo alipata fursa kuongea na Watanzania waishio Uingereza katika mwaliko
rasmi kutoka serikali ya Uingerza. Katika ziara yake nchini Uingereza Mh
Sospeter Muhongo ameambata na Bw. Athanas Macheyeki, Bw. Seleman Hatibu na Bw. Sosthenes
Massola.
Mh. Muhongo aliwaeleza Watanzani suala zima
la gas na jinsi gani serikali itavyotumia gas hiyo kuleta maendeleo ya nchi.
Amesema “serikali itahakikisha kuwa kila kijiji kinapata umeme na mpaka kufikia
mwaka 2025 nchi ya Tanzania itaondoka na umasikini”. Aliendelea kusema kuwa
bila ya umeme hatutoweza kutoa umasikini hivyo wizara yake itatafuta miundo
mbinu ya kisasa ili kuwezesha suala zima la matatizo ya umeme linaondoka. Pia
amesema wizara yake itaangalia tena ufumo wa Tanesco na kuanzisha idara zingine
ambazo zitashirikiana na zitawezesha kutatua matatizo yanayoikabili Tanesco.
Vilevile Mh Muhongo aliwataka wawekezaji wa
Kitanzania waweze kuwekeza katika sekta ya nishati na madini.
Habari na Ally Muhdin- London
1 comments:
Safi. Ufupisho makini- baada ya hotuba ndefu aliyofanya kwa saa nne bila kupumzika!
Post a Comment