BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Monday, 4 March 2013

Mkutano wa CDM UK


Mh Mpenda Maendeleo,

Tunakusalimu sana tukiwa na tegemeo kwamba ujumbe huu unakufikia ukiwa katika afya njema. Tunakutumia ujumbe huu kwani tumejiridhisha una sifa kubwa moja na ya pekee ya u-Tanzania inayotakika katika kulikomboa na kuliimarisha taifa la Tanzania kifikra na kiuchumi. Nyongeza ya hapo, tumewaza na kujiridhisha kwamba wewe unastahiri heshima ya kukaribishwa katika mkutano wa ki-historia utakaohutubiwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, Naibu katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbuge wa Jimbo la Ubungo Mh John John Mnyika. Tunakupa heshima ya pekee hii tukiwa na imani kubwa kwamba wewe ni mpenda maendeleo mbadala ya nchi yako (asilia) ya Tanzania, kwa hiyo  mchango wako wa kimawazo utasaidia katika kazi hii ya ukombozi wa kifikra na kiuchumi unaotukabiri. 

Kama tumekosea katika kuwaza na kudhania una sifa zilizotajwa hapo juu, Basi tunakuomba sana utuwie radhi na tukutakie kazi njema na maisha mema katika shughuli zako zenye tija.

Mkutano wetu utafanyika siku ya jumamosi Tarehe 9th March 2013 mahali hapa, www.hotelshoreditch.com  kuanzia saa Tisa (15:00hr) mchana. Kwa habari zaidi tafadhali tembelea hapa, http://chademauk.org.uk/uchaguzi-wa-viongozi-chadema-uk/

Tunakuthamini sana

Uongozi wa CDM UK.

"Maendeleo ya kweli kwa Mtanzania yataletwa na si wenye kuelewa tu bali wenye kufahamu na kujua maendeleo katika upana wake, [DRAP, 2013]" 

0 comments:

Search This Blog