BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Monday, 4 March 2013

Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA


Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.

Source: JamiiForums 

0 comments:

Search This Blog