Watanzania waishio nchini Uingereza siku ya
Jumanne tarehe 27 March walipata fursa ya kukutana na Naibu spika wa Bunge la
Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai. Katika ziara hiyo Mhe. Ndugai alifuatana na
Mhe. Beatrice M Shellukindo, Mhe. Salehe Pamba, Mhe. Godfrey Zambi na Saidi
Yakubu.
Watanzania waishio nchi Uingereza walipata
kuuliza maswali mbalimbali kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo na kiuchumi yanayoikabili
Tanzania kwasababu walishindwa kupata majibu ya maswali hayo kupitia katika
vyombo vya habari.
Watanzania hao walitaka kujua hali halisi
kuhusu suala la Gesi linaloikabili mkoa wa Mtwara, Elimu, Katiba ya nchi na
vyombo vya habari jinsi gani vinavyofanya kazi.
Mhe. Ndugai alisema kuwa serikali inajitahi
kuelewesha wananchi wa Mtwara kuhusu suala la Gesi na kutatua migogoro iliyopo
baina ya Serikali na wananchi hao. Akongezea kujibu swali hilo Mhe Godfrey
Zambi alisema kuwa endapo wananchi wa Kusini wakisema Gesi ni ya kwao peke yao
na endapo kila mkoa ukisema unapopata rasimalimali ni yao peke yao tutaweza
kujenga nchi? Mhe. Zambi alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujua kuwa sisi sote
ni wamoja na kila kilichopo na kinachopatika katika mkoa mmoja basi ni cha nchi
nzima na si cha mkoa mmoja na kufanya hivyo basi tutaweza kujenga nchi. Mhe.
Zambi alisema kuwa serikali itawachukulia hatua viongozi waliohusika kuleta
migogoro baina ya wananchi na serikali.
Mheshimiwa Salehe Pamba alijibu suala
linakabili vyombo vya habari, alisema kuwa suala hilo serikali inaunda mikakati
ili kutatua suala hilo kwani wananchi wengi waishio nchi za nje wamesema kuwa
habari wanazozipata si sahihi na ambazo zinaleta utata katika masuala mengi ya
kujenga. Watanzania hao walisema kuwa mfano suala la Rais wa China XI Jinping
kutembelea nchini Tanzania mara baada ya kuapishwa, vyombo vingi vya habari
vimesema Tanzania imeshauzwa, naa kwa kuwa hakuna habari nyingine walizozipata kupitia
serikalini Watanzania wengi waishio nje ya nchi waliamini habari hizo ambazo si
za kweli. Mhe. Pamba alisema serikali itajadili na kuleta uvumbuzi katika uhuru
wa habari na sheria ya kulinda habari nchini Tanzania.
Akijibu suala la katiba Mheshimiwa Beatrice
M Shellukindo alisema kuwa Watanzania waishio nje ya nchi wanatakiwa kutoa
mawazo katika kuitengeneza katiba mpya ambayo itawasaidia kujenga nchi. Akiongezea
kujibu suala la katiba Naibu spika Job Ndugai alisema kuwa katiba yetu haipo
sawa na inahitaji marekebisho makubwa. Akitolea mfano nchi ya Kenya alisema
kuwa hivi sasa katiba ya Kenya ni nzuri na inawapa mafanikio makubwa katika
kujenga nchi yao. Na alitaka Watanzania waige mfano wa katiba ya Kenya ili
waweze kuinufaisha nchi yao.
Mhe. Ndugai aliwataka Watanzania wajitokeze
kwa wingi katika kutoa mchango wao wa kuchangia katiba kwani kufanya hivyo
kutasaidia kujenga nchi yao. Akimalizia aliwashukuru Watanzania waliojitokeza
kwenda kukutana na yeye pamoja na msafara wake na amewataka waendelee na
msimamo huo endapo watakapokuja viongozi wengine. Kutoka nchini Tanzania.
Habari na Ally Muhdin - London
0 comments:
Post a Comment