Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa,Navi Pillay,
amelaani mashambulizi mabaya yaliyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi au
Albino nchini Tanzania ikiwemo mauaji ya mtoto mvulana.Serikali inapaswa kukomesha mauaji hayo pamoja na unyanyapaa
dhidi yao , alisema Bi Pillay.
Muaji ya kinyama
yanayofanyiwa watu hao huhusishwa na ushirikina , kulingana na UN.
Mnamo mwaka 2010,
Salum Khalfani alikuwa mtu wa kwanza mwenye ulemavu huo kuchaguliwa kama mbunge
nchini Tanzania.
Bi Pillay alisema kuwa
watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama mtu yeyote ule bila hofu
ya kuuawa au kubaguliwa.
Katika taarifa yake,
Bi Pillay alisema kuwa mashambulizi manne ya watanzania wenye ulemavu wa ngozi,
yaliripotiwa katika siku kumi na sita kati ya mwezi Januari na Februari.
Ni pamoja na mauaji ya
mtoto mwenye miaka saba, Lugolola Bunzari. Watu walimvamia walikata paja la
uso, mkono wake wa kulia , bega la kushoto.
Babu ya kijana huyo,
mwenye umri wa miaka 95, pia aliuawa kwenye shambulizi hilo, alipojaribu
kumuokoa mjuu wake.
Bi Pillay alisema mashambulizi kama haya ni mabaya na watu wana
haki ya kuishi kama watu wengine bila hofu ya kuuawa au kujeruhiwa vibaya.
Source:BBC
Source:BBC
0 comments:
Post a Comment