Mahakama ya juu nchini Kenya hii leo itatoa uamuzi
ikiwa ina uwezo wa kusikiliza kesi iliyowasilishwa kwake na makundi ya kijamii
yakitaka tume huru ya uchaguzi nchini Kenya kusitisha shughuli ya kuhesabu kura
za urais inayoendelea katika ukumbi wa Bomas.
Makundi
hayo yanadai kuwa tume inakwenda kinyume na katiba ambayo ambayo inasema kura
zinapaswa kuhesabiwa kwa njia ya elektroniki.
Pia
Muungano wa Cord wake mmoja wa wagombea wa urais Raila Odinga umedai kuwa tume
hiyo inafanya hujuma katika shughuli ya kujumlisha kura za urais katika ukumbi
wa Bomas.
Hapo
jana Muungano wa CORD ulielezea malalamishi kuhusu shughuli yakujumlisha kura
za urais na kusema hauna imani nayo kwani ina ushahidi kuwa hujuma imefanyika
wakidai wizi wa kura.
Pia
wanadai kuwa katika baadhi ya maeneo, kura zilizopigwa ni nyingi kuliko idadi
ya wapiga kura waliosajiliwa.
Madai
haya waliyatoa hapo jana ingawa mkuu wa tume ya uchaguzi aliyakanusha vikali na
kusema hakuna mahala popote ambapo wameshuhudia matokeo kuhujumiwa.
Chama
hicho pia kilidai kuwa baadhi ya matokeo yalikuwa juu ikilinganishwa na idfadi
ya wapiga kura.
Na
kwa hilo, mkuu wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan pia alikanusha vikali akisema
hawajapata matokeo kama hayo.
Tume
hiyo imesisitiza kuwa shughuli ya kuyahakiki matokeo inafanywa mbele ya
maajenti wa vyama vyote.
Wakati
huohuo tume hiyo imekiri kuwa kulikuwa na tatizo la mtambo wake wa kupeperusha
matangazo ikisema kuwa ilikuwa inaongeza mara nane kura zilizoharibika.
Washika
dau wengi walieleza wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya kura zilizoonekana
kuharibika kwani zilikuwa kura zaidi ya laki tatu. Lakini kufikia sasa
zimepungua na kufika themanini.
Mkuu
wa tume hiyo, Issack Hassan alisema kuwa komputa ilikuwa inaongeza idadi ya
kura zilizoharibika kwa mara nane.
Shughuli
ya kukusanya matokeo ilianza upya kwa mikono kufuatia matatizo haya lakini
Uhuru Kenyatta angali anaongoza dhidi ya Raila Odinga.
"kulikuwa
na makosa kwa namna ambavyo programu ya komputa ilikuwa imeundwa, '' alisema
Hassan.
''Kwa
kura zote zilizoharibika kwa kila mgombea zilikuwa zinaongezeka mara nane ,''
aliongeza kusema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment