Matokeo ya
mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda
na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema
Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu
hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada yawakenya
kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea
kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya
uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila
Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika
mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa
mwaka wa 2007.
Waandishi wa BBC wanasema iwapo
Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri
Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo
rasmi ya mshindi baadaye leo
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa
uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya
kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa
hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe
ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa
amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie
maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku
ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
0 comments:
Post a Comment