BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Wednesday, 14 April 2010

Katie Price Kutoshiriki mbio za Marathon


Mrembo maarufu nchini Uingereza ametangaza kujitoa katika mashindano ya mbio za Marathon. Amefikia uamuzi huo wakutangaza kujiuzulu kupitia tovuti yake lakini hatutamka sababu za ugonjwa ambao unaomfanya aache kukimbia mbio hizo za Marathon.

Uamuzi wa kujito umewafanya watu wawe na tetesi kuwa labda ana mimba ya mtoto wa nne.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema wazi kuwa anajaribu kutafuta mtoto mwingine na mume wake mpya Alex Reid, 34.

Gazeti la OK! limeandika kuwa ameonekana nje ya Hospitali ya Portland huku akiwa ameshikilia tumbo lake.

Price amesema kwenye tovuti yake " Hatoweza kushiriki mbio za Virgin London Marathon kwa mwaka huu."

Aliongezea "nimeweza kufanya mazoezi vizuri na nilikuwa natarajia kukimbia mbio hizo mwaka huu kwaajili ya kuchangisha pesa za chama cha vipofu ( wasioona) lakini doctors wamenishauri nisishiriki mbiyo hizo." Nawatakia kila kila la kheri washiriki wote wa mbio hizo za Marathon.

Reid ambaye alishiriki katika kipindi cha Asubuhi Hii alipoulizwa na mtayarishaji wa kindindi hicho Philip Schofied and Holly Willoughby kama Price ana mimba alijibu kwa kuonyesha na kufunga mdomo wake na kusema "labda inawezekana labda haiwezekani"

Price kama kweli ana mimba basi itakuwa mimba ya mtoto wa nne, tayari anawatoto watatu ambao amezaa na Peter Andre watoto wawili na mmoja amezaa Dwight York.0 comments:

Search This Blog