BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Friday, 16 April 2010

Manchester United yaelekea kupoteza ubingwa

Timu ya Manchester United ambayo inaonekana kuelekea kupoteza ubigwa wa ligi ya Uingereza wana mechi ngumu na majirani zao Manchester City siku ya Jumamosi.


Timu hiyo ambayo hivi karibuni ilitolewa katika king'ang'aniro cha kugombea kombe la mabingwa wa Ulaya, vile vile kupoteza michezo miwili muhimu ya ligi kuu ya Uingereza.Ilifungwa mabao mawili na Chelsea na kutoka sare ya bila bila na Blackburn Rover.

Ukiangalia ligi hiyo ambayo inafikia ukingoni ambapo timu karibia zote zimebakiza mechi nne, Chealse inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa huo japokuwa wana mechi mbili ngumu, Inatakiwa ikacheze Tottenham katika uwanja wa White Hart Lane na Liverpool katika uwanja wa Anfield.

Tegemeo kubwa la timu ya Manchester United, Wayne Rooney ameumia na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kushindwa kupata ushindi katika mechi zake za hivi karibuni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameifungia timu yake magoli yasiyozidi 36, na anaoneka kuwa pengo kubwa sana kwa timu hiyo.

Dimitar Berbatov anaonekana bado hajaonesha makali yake, kwani wapenzi wengi wanampinga kutokana na jinsi anavyocheza. Inabidi afanye juhudi za kuweza kuipatia Manchester United magoli yenye kuiwezesha kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.

0 comments:

Search This Blog