BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Welcome - Karibu

Wedding Photography and Video

Sunday, 18 April 2010

Ubingwa Bado Uko Wazi
King'ang'aniro cha kugombea ubingwa wa ligi nchini Uingereza bado kiko wazi kutokana na matokeo ya michezo ya jana.

Chelsea ambayo inaongoza ligi hiyo iliweza kupoteza mchezo wake muhimu sana ilipofungwa na Tottenham 2-1.

Nayo timu ya Manchester United imeweza kujiweka katika nafasi nzuri katika kutetea taji baada ya kuwafunga majirani zao Manchester City 2-1. Ushindi huo umewawezesha kutofatiana na Chealsea katika kuongoza ligi kwa pointi moja.

Goli pekee la Manchester United lilifungwa katika dakika za nyongeza na kiungo mkongwe Paul Scholes.

Scholes alikuwa peke yake ndani ya kumi na nane na kuweza kufunga goli la kichwa, lililowapa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo moyo wa kuchukua ubingwa kwa mara nyingine tena.

Alex Fergurson alifurahi ushindi huo na kusema kwamba timu yake imeweza kufunga magoli dhidi ya Manchester City katika dakika za mwisho mara tatu.


0 comments:

Search This Blog