Mwanamuziki wa kizazi kipya 50 cent inasemekana amewekeana mkataba na Gamu Nhengu ambaye alishindwa kuendelea katika mashindano ya X-factor.
Gamu Nhengu atajulikana kwa jina la Miss Gamuchirai katika kampuni ya G-Note records inayomilikiwa na 50 Cent.
Miss Gamuchirai atajihusisha na muziki wa Pop and RnB ingawa G-Note records inajihusisha sana na muziki wa Hip Hop.
Ingawa kampuni nyingi zilijitokeza kuingia mkataba na Miss Gamuchirai, lakini Miss Gamuchirai amekubali kuingia mkataba na G-Note records kutokana na manufaa ya mkataba kwa mwanamuziki huyo.
Source: Ally Muhdin
0 comments:
Post a Comment