Mwimbaji maarufu nchini Uingereza Cheryl Cole ameshika nafasi ya kwanza kati ya warembo maarufu mia moja wa FHM's duniani. Cheryl ameshikilia nafasi hiyo kwa mara ya pili mfululizo sasa.
Mcheza sinema Megan Fox pamoja na Marissa Miller walishindwa kuchukua nafasi hiyo yenye kugombewa na warembo wengi duniani.
Cheryl ambaye ameatengana na mumewe mchezaji wa timu ya Chelsea Ashley Cole, inasemekana kuwa mumewe alifanya mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine.
Ijapokuwa alipata matatizo katika ndoa yake lakini aliweza kushika nafasi hiyo ya kwanza na nafasi ya pili kushikiliwa na mcheza tamthilia ya Transformers Megan Fox na nafasi ya tatu kuchukuliwa na mwanamavazi maarufu ya Victoria Secret Merissa Miller.
Mchezaji wa tamthilia ya Twilight Kristen Stewart ameshikilia nafasi ya sita, Kelly Brook ambeye aliwahi kushika nafasi ya kwanza ametokea kuwa katika kumi bora.
Thursday, 29 April 2010
Cheryl Cole Achaguliwa kuwa mrembo
Posted by Ally Muhdin at 08:05 0 comments
Thursday, 22 April 2010
Ryan Air Yakataa Kuwalipa Abiria
Ndege hiyo yenye kubana matumizi imesema kuwa haitalipa malipo ya nyumba za kulala wageni pamoja na gharama za chakula.
Bw. O'Leory amesema kuwa abiria wote watarudishiwa gharaza za tiketi na siyo gharama nyingine zozote.
Ryanair kwa siku inabeba abiria wasiopungua 220,000 wa nchi za Ulaya, Lakini Bw. O'Leary amesema hajui abiria wangapi wameathirika na matatizo hayo.
Waziri wa mambo ya Nje nchini Uingereza Bw. David Milliband amesema kuwa mashirika ya ndege yanabidi kuwapa abiria gharama za chakula na makazi ya kulala kwa wale walioathirika na maafa hayo.
Bw. Milliband amesema kuwa itakuwa si kitendo kizuri kama mashirika ya ndege hayatoa huduma hizo.
Wizara yake inajitahidi kuwasaidia raia wate walikumbwa na matatizo ya usafiri vilevile wanajitahidi kuhakikisha shule hazitotoa adhabu kwa wanafunzi wakakao kosa kufanya mitihani kutokana na matatizo ya usafiri.
Posted by Ally Muhdin at 09:17 0 comments
Tuesday, 20 April 2010
Viwanja Vya Ndege Vyafungwa
Posted by Ally Muhdin at 08:34 0 comments
Monday, 19 April 2010
TANGAZO KWA WANA-LONDON
Viongozi wa muda wa Jumuiya ya watanzania London inawaomba watanzania wote waishio London kuhudhuria mkutano wa wana-London utakaofanyika ubalozini siku ya jumamosi tarehe 24-April-10 kuanzia saa 1100 asubuhi. Mkutano huu unategemea kuongelea maswala ya chaguzi wa viongozi na muundo mzima wa jumiya ya London.
Uchaguzi wa viongozi wa London unategemewa kufanyika tarehe 01-May-10. Mawazo yako ni mchango mkubwa kwa jumuiya na kama unazo sifa za uongozi na ari ya kuendeleza jumuiya mlango uko wazi kwa kila mmoja.
Posted by Ally Muhdin at 09:23 0 comments
Sunday, 18 April 2010
Ubingwa Bado Uko Wazi
Posted by Ally Muhdin at 10:49 0 comments
Saturday, 17 April 2010
Elizabeth Taylor Achumbiwa
Dame Elizabeth Taylor ataolewa kwa mara ya nane katika kumbukumbu za maishani mwake.
Habari zinasema kwamba muigizaji huyo maarufu wa tamthilia asiyepungu chini ya umri wa miaka 78 na mpenzi wake wa siku nyingi Jason Winter mwenye umri wa miaka 49 hivi karibuni walikula kiapo cha kuwa pamoja.
Marafiki wa karibu wanasema kuwa "Hakuna kitu cha kuficha wamekuwa pamoja milele na wanapendana... Hivi sasa waimarisha mapenzi yao"
Taylor hivi karibuni alizungumza kwa wazi kuhusiana na jinsi gani anavyompenda Winters, ambaye muda si mrefu tangu awe mkurugenzi wa Janet Jackson's.
Taylor alisema bila kuficha kuwa Jason Winters "Ni mmmoja kati ya wanaume wa ajabu aliowapata kuwajua"
Posted by Ally Muhdin at 07:44 0 comments
Friday, 16 April 2010
Ashikiliwa na Polisi kwa kosa la Kumtisha Cherly Cole
Posted by Ally Muhdin at 19:21 0 comments
Manchester United yaelekea kupoteza ubingwa
Timu ya Manchester United ambayo inaonekana kuelekea kupoteza ubigwa wa ligi ya Uingereza wana mechi ngumu na majirani zao Manchester City siku ya Jumamosi.
Posted by Ally Muhdin at 07:39 0 comments
Wednesday, 14 April 2010
Katie Price Kutoshiriki mbio za Marathon
Mrembo maarufu nchini Uingereza ametangaza kujitoa katika mashindano ya mbio za Marathon. Amefikia uamuzi huo wakutangaza kujiuzulu kupitia tovuti yake lakini hatutamka sababu za ugonjwa ambao unaomfanya aache kukimbia mbio hizo za Marathon.
Uamuzi wa kujito umewafanya watu wawe na tetesi kuwa labda ana mimba ya mtoto wa nne.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema wazi kuwa anajaribu kutafuta mtoto mwingine na mume wake mpya Alex Reid, 34.
Gazeti la OK! limeandika kuwa ameonekana nje ya Hospitali ya Portland huku akiwa ameshikilia tumbo lake.
Price amesema kwenye tovuti yake " Hatoweza kushiriki mbio za Virgin London Marathon kwa mwaka huu."
Aliongezea "nimeweza kufanya mazoezi vizuri na nilikuwa natarajia kukimbia mbio hizo mwaka huu kwaajili ya kuchangisha pesa za chama cha vipofu ( wasioona) lakini doctors wamenishauri nisishiriki mbiyo hizo." Nawatakia kila kila la kheri washiriki wote wa mbio hizo za Marathon.
Reid ambaye alishiriki katika kipindi cha Asubuhi Hii alipoulizwa na mtayarishaji wa kindindi hicho Philip Schofied and Holly Willoughby kama Price ana mimba alijibu kwa kuonyesha na kufunga mdomo wake na kusema "labda inawezekana labda haiwezekani"
Price kama kweli ana mimba basi itakuwa mimba ya mtoto wa nne, tayari anawatoto watatu ambao amezaa na Peter Andre watoto wawili na mmoja amezaa Dwight York.
Posted by Ally Muhdin at 00:14 0 comments
Tuesday, 13 April 2010
Marehemu Seifu Nassor
Posted by Ally Muhdin at 19:54 0 comments
Adebayor ajiuzulu kuchezea timu ya Togo
Mshambuliaji maarufu wa timu ya Manchester City Emmanuel Adebayor ametangaza rasmi kujiuzulu kucheza mechi za kimataifa na kuichezea timu yake ya taifa ya Togo.
Adebayor amechukua uamuzi huo baada ya timu yake ya Togo kushambuliwa walipokuwa katika mashindano ya kombe la Africa nchini Angola.
Timu hiyo ya Togo ilishambuliwa na kusababisha watu watatu kupoteza kufariki.
Akitoa maelezo na sababu za kujiuzulu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema "Kutokana na tukio la shambulizi na ugaidi ambalo limesababisha watu wawili wa nchi mwake kupoteza maisha hiyo ndiyo sababu iliyomfanya kuchukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu kucheza mechi za kimataifa"
Akiendelea kutoa maelezo yake alisema kuwa "sisi ni wachezaji mpira tumeenda kucheza mpira na kuiwakilisha nchi yetu, lakini tumevamiwa na watu wanaotaka kupoteza maisha yetu, sitoweza kusahau na sihitaji kutokewa tena na kitendo hicho katika maisha yangu".
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Cabinda nchini Angola. Magaidi waliivamia timu hiyo ya Togo na kuanza kurusha risasi. kitendo hicho kilisababisha mwalimu msaidizi na mwandishi wa timu ya Togo kupoteza maisha, pia dereve wa basi alipoteza maisha. vile vile beki wa timu hiyo Serge Akakpo na mlinda mlango Kodjovi Obilale kuumia. kundi la "The Front for the Liberation of the enclave of Cabinda" linashutumiwa kwa shambulio hilo lakini kundi hilo limekataa kuhusika na shambulio hilo.
Habari na Ally Muhdin, www.tz-one.blogspot.com
Posted by Ally Muhdin at 14:09 0 comments
Carragher Awajibu wapenzi wa soka
Jamie Carragher amejibu usemi wa wapenzi wengi wa mpira wa miguu ya kuwa Liverpool itapigwa na pengo kubwa itakapokosa kufaulu kucheza mashindano ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.
Timu hiyo inayotokea Anfield imeanza kukubaliana na matokea kama kuna uwezekano wa kushindwa kucheza kombe hilo la mabigwa wa ulaya ambolo wameweza kufanikiwa kucheza kombe hilo kwa muda wa miaka saba mfululizo.
Wekundu hao wanashikilia nafasi ya sita katika ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare na Fulham siku ya jumapili na wapo pointi sita nyuma ya Manchester City katika kugombea nafasi ya nne, vilevile wamecheza mechi zaidi.
beki huyo wa siku nyingi amesema haoni sababu yoyote kwanini wasiweze kurudi na kuwa na nguvu kubwa zaidi.
'Hakuna kitu kipya kama hatutofanilkiwa, kwani tumeshawahi kucheza na watu wanasahau hivyo' Alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.
'kama hatutofaulu msimu huu ninauhakika msimu ujao hautakuwa mbaya kama msimu huu'.
Carragher aliongezea kwa kusema: 'Tumeuanza msimu vibaya jambo ambalo hatukulitaraji. Tulipenda kushiriki kombe la mabingwa wa ulaya kuliko kombe la ulaya.
Kwa upande wangu kushinda vikombe ndiyo maana ya mashindano na ndiyo mchezo wenyewe, lakini kuna kushindwa pia katika mashindano.
Habari na Ally Muhdin, www.tz-one.blogspot.com
Posted by Ally Muhdin at 13:57 0 comments
Portsmouth kuomba kibali

Portsmouth wanafanya mpango wa kukiomba chama cha mpira nchini Uingereza kiballi cha kucheza kombe la barani ulaya.
Timu hiyo ambayo imeshuka daraja imeweza kujipatia nafasi ya kushirika katika kombe hilo baada ya kuweza kufika fainali za kombe la shirikisho la soka nchi Uingereza ambapo itapambana na Chelsea tarehe 15 May. Timu hiyo iliitoa Tottenham siku ya jumapili.
Portsmouth haitakiwi kushiriki mashindano hayo baada ya kushindwa kuomba kibali hicho, mwisho wa kuomba kibali hicho ulikuwa mwezi wa March 1.
Andrew Andronikou amesema kuwa kuweza kushiriki kwenye mashindano hayo kuleta changamoto kwa wanunuzi wanaotaka kununua timu hiyo. Watafanya kila njia kuweza kufanikisha mashindano hayo kufanyika Fratton Park. kushinda mechi yake
"Nafikiri ni muhimu kuweza kufikilia na kutumia njia zote za kuweza kucheza kombe la Ulaya" Andronikou alisema.
"Inajizungumza yenyewe, itakuwa bora zaidi na mafanikio makubwa kwa timu yetu na kuwavutia wanunuzi wa timu."
Kama watafanikiwa, Portsmouth watachukua nafasi katika ligi ya Ulaya kama washindi wa kikombe cha chama cha mpira nchi Uingereza FA na itaweza kuwaongezea kipato msimu ujao.
Wataki huohuo timu hiyo inataka kuzungumza na timu ya Lens yenye makazi yake nchini Ufaransa kuhusu mchezaji Dindane.
Aruna Dindane mkataba wake ni kuichezea Portsmouth mechi 21, siku ya nusu fainali ndiyo mechi yake ya 21, lakini kama ataendelea kuichezea timu hiyo mechi nyingine itawaghalimu Pompey malipo ya £4
Andronikou anauhakika watafakinikiwa maafikiano na timu hiyo ya Kifaransa.
Habari na Ally Muhdin, www.tz-one.blogspot.com
Posted by Ally Muhdin at 13:44 0 comments
Sunday, 11 April 2010
Al-HUDAA
Posted by Ally Muhdin at 10:54 0 comments
Saturday, 10 April 2010
Amani Awafurahisha Wapenzi wa Muziki jijini London
Mwimbaji maarufu nchi Kenya, Amani kwa mara nyingine tena aliwafurahisha wapenzi wa muziki jijini London. Amani ambaye yupo nchini uingereza kwa ziara mwezi mmoja, alifanya show yake yake tatu katika ukumbi wa Club Africa iliyopo Canning Town, London. Show hiyo ilionekana imefana sana kwani wapenzi wengi walionekana kuridhika na minenguo na kipaji cha uimbaji cha mwanadada huyo. Mwandishi wetu alipowahoji wapenzi wa mwanadada huyo, walisema kuwa sauti ya mwanadada huyo na mashahiri ya nyimbo zake zimefawanya waridhike na tamasha hilo. Vilevile unenguwaji wa mwanadada huyo umewaridhisha sana.
Posted by Ally Muhdin at 09:31 0 comments
Sunday, 4 April 2010
Saturday, 3 April 2010
Posted by Ally Muhdin at 23:53 0 comments
Posted by Ally Muhdin at 23:45 0 comments
Posted by Ally Muhdin at 23:40 0 comments
Posted by Ally Muhdin at 23:12 0 comments
Posted by Ally Muhdin at 22:45 0 comments









